Jumapili, 15 Desemba 2019

Vifo kutokana na utoaji mimba

Duniani, inakadiriwa vitendo vya utoaji mimba milioni 46 hufanyika kila mwaka na mara nyingi wanawake hunusurika, hata kama sehemu kubwa ya vitendo hivyo haviruhusiwi kisheria. Lakini utoaji mimba usiyo salama unaweza kusababisha kifo, au matatizo mengine kama vile maambukizi, maumivu ya kudumu, na ugumba.
Wanawake wanapokata tamaa mara nyingi hujaribu kutafuta njia za kukatisha ujauzito. Epuka njia zifuatazo. Ni hatari sana.
Epuka utoaji mimba usiyo salama. Jaribu kuzuia mimba isiyotakiwa kabla haijatokea.
  • Usiingize vifaa vyenye ncha kali kama vile vijiti, waya au mirija ya plastiki ukeni au kwenye kizazi (tumboni). Vitu hivyo vinaweza kutoboa au kujeruhi tumbo na kusababisha kuvuja damu na maambukizi hatari.
  • Usiweke dawa za mitishamba au mimea ukeni au tumboni. Vitu hivyo vinaweza kuunguza au kukudhuru vibaya, na kusababisha uharibifu wa viungo vya ndani, maambukizi, na uvujaji damu.
  • Usiweke vitu kama vile vinavyobabua, majivu, sabuni, au mafuta ya taa ukeni au tumboni. Pia kamwe usinywe vitu hivyo.
  • Usitumie dawa au tiba za asili katika vipimo vikubwa ili kutoa mimba (iwe kwa njia ya mdomo au kupitia ukeni). Kwa mfano, kutumia dawa nyingi ya malaria (krolokwini) au dawa za kusimamisha damu kutoka baada ya kujifungua (ergometrine, oxytocin) kunaweza kusababisha kifo hata kabla mimba haijatoka.
  • Usipige tumbo lako au kujirusha chini kwenye ngazi. Hii inaweza kusababisha majeraha na uvujaji damu ndani ya mwili wako, lakini usisababishe mimba kutoka.

Maoni 3 :

  1. Ubarikiwe kwa kutoa somo hili limenifanya nijue mambo mengi ambayo nilikuwa sina majibu nayo na ambayo baadhi yapo kwenye jamii inayotuzungua na mimi kupitia somo hili nitaweza kuelimisha wengine.
    Pia nilikuwa naomba kujua kama mama mwenye tatizo la ugonjwa wa kisukari je anaweza kubeba ujauzito na kuweza kujifungua mtoto salama na akawa hana tatizo la ugonjwa wa huo wa kisukari?

    JibuFuta
  2. Ndio mama mwenye kisukari anaweza kushika mimba na kujifungua salama lakini anapogundua yeye ni mjamzito tu awahi katika kituo cha kutolea huduma za afya apata kuchukuliwa vipimo na uangalizi wa afya yake, maana mahudhulio yake ya kliniki hayatakuwa kama ya wajawazito wengine.

    JibuFuta
  3. Nashukuru kwa kunipatia jibu zuri ambalo pia sikuweza kuwa na hakika na jambo hili.
    Ubarikiwe sana na endelea kutoa elimu ya afya maana asilimia kubwa ya jiamii setu hawana elimu ya ayfa ya kutosha.

    JibuFuta