Alhamisi, 19 Desemba 2019

Maumivu wakati wa kujamiiana ! (dyspareunia)



Tendo la kujamiiana linapaswa kuwa tendo la kuvutia na bila shaka utajiuliza maswali mengi iwapo maumivu yataambatana na tendo hilo. Zifuatazo ni sababu zinazoweza kusababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa:

Vaginismus:
Hili ni neno la kitaalamu linalomaanisha kukaza kwa misuli ya uke kusiko kwa hiari wakati wa tendo la ndoa. Hii hutokea pale ambapo mwanamke anakua na hofu ya kuumizwa wakati wa kuingiliwa.
Maambukizi katika uke:
Hii hutokea mara kwa mara pale ambapo uke unashambuliwa na vijidudu kama vile fangasi. Hatimaye sehemu iliyo na maambukizi huweza kuwa na maumivu wakati wa kujamiiana.
Uvimbe katika mji wa mimba:
Iwapo kuna uvimbe katika mji wa mimba (Uterus) kama vile uvimbe unaofahamika kitaalamu kama fibroids, huweza kusababisha maumivu wakati wa kujamiiana hasa pale mwanamke anapoingiliwa kwa nguvu (deep penentration).
Ukavu katika uke:
Hii hutokea iwapo mwanamke hajaandaliwa vizuri kabla ya kuingiliwa hivyo hukosa msisimko wa kutosha kuzalisha majimaji yanayolainisha uke. Pia huweza kusababishwa na hofu wakati wa kujamiiana hali inayopelekea mwanamke kutoshiriki kikamilifu na kukosa msisimko. Hali ya kukoma kwa hedhi pia husababisha ukavu ukeni kutokana na kukosekana kwa homoni mbalimbali. Yote haya huweza kusababisha maumivu wakati wa kujamiiana.
Majeraha:
Mwanamke anaweza kuhisi maumivu wakati wa kujamiiana iwapo bado hajapona majeraha yatokanayo na kujifungua, upasuaji au ubakaji.
Maumivu wakati wa kujamiiana huweza kutibiwa kutegemea chanzo cha tatizo. Mwanamke anapaswa kusubiri walau wiki sita baada ya kujifungua kabla ya kujamiiana tena. Iwapo shida ni ukavu ukeni, ni vema kutumia vilainishi visivyo na kemikali (water-based lubricants). Iwapo ukavu unasababishwa na ukomo wa hedhi, ni vema kuwasiliana na daktari akuandikie dawa za estrojeni au madawa mengine.

Ni vizuri pia kuondoa mawazo ya kujilaumu (guilt) au hisia za matukio mabaya ya nyuma kama ubakaji. Maumivu yakiambatana na dalili kama kutoka damu, hedhi zisizoeleweka, ute usio wa kawaida au kukaza misuli ya uke kusiko kwa hiari ni vema kumtembelea daktari kwa msaada zaidi.

Je nitajuaje kama ninafangasi ukeni?



1.Kuwashwa kunakoambatana na maumivu ukeni.
2.Maumivu kama unaungua na moto wakati wa kukojoa au kufanya mapenzi.
3.Kutokwa na uchafu mweupe, mzito, uliogandiana, usio nharufu na unaofanana na jibini (cheese).

“Ni muhimu kumuona daktari uonapo dalili hizi au zaidi kwa ajili ya uchunguzi na matibabu sahihi.





Je,Una hofu kwa sababu umechelewa kuona siku zako, na unajua wewe si mjamzito?


Kuchelewa kuona siku zako au kuzikosa hutokea kwa sababu mbalimbali tofauti na ujauzito.


Wanawake wengi huona siku zao baada ya siku 28. Ingawa mzunguko wa hedhi kawaida huweza kutumia siku 21 hadi siku 35. 

Ikiwa hujapata hedhi katika kipindi hiki, zifuatazo huweza kuwa visababishi:

  • Msongo wa mawazo
  • Uzito mdogo au uliokithiri.
  • Vidonge vya uzazi wa mpango.
  • Magonjwa ya kudumu & ya muda mrefu.
  • Magonjwa ya tezi ya thyroid

Uke wangu hauingiliki. Je, nina tatizo gani ? (Vaginismus)


Takwimu zinaonesha kati ya wanawake 100 duniani, hadi wanawake 17 wanasumbuliwa na tatizo hili.
Vaginismus ni tatizo la kukaza kwa misuli ya sehemu ya juu ya uke pale ambapo kitu chochote kinapojaribu kupenya au kukandamiza uke. Hali hii huweza kuambatana na maumivu yanayoweza kuwa ya kawaida au makali sana na mwanamke husika hawezi kujizuia kukaza kwa misuli hii.
Pia, vaginismus inaweza kumpata mwanamke wa umri wowote, kuanzia vijana wadogo hadi walioko katika ndoa.


Chanzo na Dalili: Chanzo cha tatizo hili hakijafahamika lakini huhusianishwa zaidi na hofu ya kujamiiana kutokana na sababu za kihisia au kibaiolojia.
Sababu za kihisia ni kama:
  • Hofu kwa mfano hofu ya maumivu au kupata mimba.
  • Wasiwasi au hatia.
  • Ugomvi katika mahusiano au mwenza mkorofi.
  • Matukio kama ubakaji.
Sababu za kibaiolojia:
  • Maambukizi kama maambukizi ya njia ya mkojo (UTI) au fangasi.
  • Cancer
  • Kujifungua
  • Kukoma hedhi
  • Upasuaji wa nyonga
  • Athari za madawa.
Dalili zake ni kama vile:
  • Maumivu wakati wa kujamiiana kama hisia ya kuchanika kuta za uke.
  • Mwanaume anakua kama anakutana na ukuta usiopenyeka wakati wa kujamiiana.
  • Maumivu wakati wa kufanyiwa vipimo ukeni.
  • Kukaza kwa misuli ya uke au kuacha kupumua wakati wa kuingiliwa (intercourse)
Tatizo hili linaweza kutibika kwa njia ya kujizoesha kwa namna mbili. 
Kwanza, kwa kufanya mazoezi ya Kegeli (Kegel Exercises) ambapo mhusika hukaza na kulegeza misuli inayohusika kuzuia mkojo ili kujijengea maamuzi juu misuli hii.
Pili, kwa msaada wa daktari au mtaalamu wa mambo ya wanawake, vifaa maalumu vya ukubwa mbalimbali (Vaginal Dilators) huingizwa ukeni ili kuuzoesha uke na kuondoa hali ya woga. Zoezi hili linaweza kufanywa na mhusika mwenyewe au kwa msaada wa mwenza wake kwani ni swala la kujizoesha.

Jumapili, 15 Desemba 2019

Vifo kutokana na utoaji mimba

Duniani, inakadiriwa vitendo vya utoaji mimba milioni 46 hufanyika kila mwaka na mara nyingi wanawake hunusurika, hata kama sehemu kubwa ya vitendo hivyo haviruhusiwi kisheria. Lakini utoaji mimba usiyo salama unaweza kusababisha kifo, au matatizo mengine kama vile maambukizi, maumivu ya kudumu, na ugumba.
Wanawake wanapokata tamaa mara nyingi hujaribu kutafuta njia za kukatisha ujauzito. Epuka njia zifuatazo. Ni hatari sana.
Epuka utoaji mimba usiyo salama. Jaribu kuzuia mimba isiyotakiwa kabla haijatokea.
  • Usiingize vifaa vyenye ncha kali kama vile vijiti, waya au mirija ya plastiki ukeni au kwenye kizazi (tumboni). Vitu hivyo vinaweza kutoboa au kujeruhi tumbo na kusababisha kuvuja damu na maambukizi hatari.
  • Usiweke dawa za mitishamba au mimea ukeni au tumboni. Vitu hivyo vinaweza kuunguza au kukudhuru vibaya, na kusababisha uharibifu wa viungo vya ndani, maambukizi, na uvujaji damu.
  • Usiweke vitu kama vile vinavyobabua, majivu, sabuni, au mafuta ya taa ukeni au tumboni. Pia kamwe usinywe vitu hivyo.
  • Usitumie dawa au tiba za asili katika vipimo vikubwa ili kutoa mimba (iwe kwa njia ya mdomo au kupitia ukeni). Kwa mfano, kutumia dawa nyingi ya malaria (krolokwini) au dawa za kusimamisha damu kutoka baada ya kujifungua (ergometrine, oxytocin) kunaweza kusababisha kifo hata kabla mimba haijatoka.
  • Usipige tumbo lako au kujirusha chini kwenye ngazi. Hii inaweza kusababisha majeraha na uvujaji damu ndani ya mwili wako, lakini usisababishe mimba kutoka.

Kwa nini baadhi ya wanawake hutoa mimba?


Kutoa mimba kawaida ni uamuzi mgumu. Baadhi ya dini hufundisha kuwa utoaji mimba siyo sahihi na katika nchi nyingi utoaji mimba hauruhusiwi kisheria na siyo salama. Lakini kuna sababu nyingi kwa nini mwanamke anaweza kujaribu kutoa mimba. Hapa chini ni mifano kadhaa:
  • Tayari anapokuwa na watoto ambao anaweza kuwahudumia.
  • Ujauzito huo unapokuwa hatari kwa afya au maisha yake.
  • Hana mwenzi wa kumsaidia kumhudumia mtoto atakayezaliwa.
  • Anataka kwanza kumaliza shule.
  • Hataki kupata watoto.
  • Alipata mimba baada ya kubakwa.
  • Kuna mtu ambaye anamlazimisha kuitoa mimba.
  • Mtoto atazaliwa na matatizo makubwa ya kiafya au kimaumbile.
  • Ana VVU au UKIMWI.

Alhamisi, 12 Desemba 2019

Nini hufanyika unapomuona daktari kuhusu tatizo la kupata hedhi kupita kiasi ?


  • Unapomuona daktari atachukua historia ya afya yako kwa ujumla
  • Historia ya afya ya uzazi na mzunguko wako wa hedhi
  • Historia ya dawa zote unazotumia
  • Daktari atahitaji kukufanyia vipimo vya mwili ili kuangalia kama kuna kisababishi kinachochangia hedhi kutoka kwa wingi
  • Daktari naweza chukua damu kupima wingi wako wa damu , kiwango chako cha homoni za uzazi pia na vipimo vingine kulingana na alivyokuona
  • Datari anaweza kukufanyia ultrasound ili kungalia mji wa uzazi na via nyingine za uzazi kama kuna tatizo

ATHARI ZA HEDHI NZITO KUPITA KIASI KWENYE AFYA


  • Hedhi nzito kupita kiasi huchangia wanawake wengi kupata upungufu wa damu
  • Hedhi kuwa nzito kupita kiasi huweza kuwa ni dalili ambao unahitaji tiba ya haraka
  • Huweza kuchangia kudhoofisha afya ya akili ya mwanamke ikiwemo kujiamini na wasiwasi

Sababu gani huweza kuchangia mwanamke kupata hedhi nzito kupita kiasi?

Sababu gani huweza kuchangia mwanamke kupata hedhi nzito kupita kiasi?
  • Vivimbe kwenye kuta za mji wa kizazi; vivimbe hivi sio saratani huitwa fibroids
  • Yai kupevuka bila mpangilio (Irregular ovulation) ; hali hii husababisha kuta za mji wa mimba zivimbe na kuwa nene hivyo kutoa damu nyingi. Hutokea zaidi kipindi cha kuvunja ungo na kipindi cha kukaribia ukomo wa hedhi
  • Matatizo ya kugandisha damu
  • Matumizi ya dawa za kuzuia damu kuganda
  • Baadhi ya wanawake waliotumia vitanzi (IUD) hasa ndani ya mwaka wa kwanza
  • Maambukizi ya mji wa mimba na mirija ya uzazi (PID)
  • Endometriosis
  • Saratani ya mji wa kizazi; kwa kinamama waliofikia umri wa ukomo wa hedhi. Wakianza kupata hedhi isiyokoma huweza kuwa dalili ya ya saratani ya mji wa kizazi

Je ni wakati gani mwanamke anatakiwa kuhisi kuwa anapata hedhi kupita kiasi?

Je ni wakati gani mwanamke anatakiwa kuhisi kuwa anapata hedhi kupita kiasi?
  • Unapata hedhi inayozidi siku 7
  • Unapata hedhi nzito inayofanya ubadiri pedi moja ndani ya masaa mawili
  • Unapata hedhi nzito inayokulazimu kuvaa pedi zaidi ya moja
  • Unapata hedhi nzito inayolowesha hadi nguo za nje
  • Unapata hedhi nzito inayokulazimu kuamka usiku kubadiri pedi
  • Hedhi inayotoka na mabonge