1. Fahamu visababishi
• Kurithi
• Umri mkubwa
• Kupata mtoto wa kwanza baada ya umri wa miaka 35
• Uzito mkubwa
• Kutokufanya mazoezi
• Matumizi ya tumbaku au pombe
2. Fahamu hali ya kawaida kwako
• Fahamu hali ya kawaida ya matiti yako kwa kujitazama kwenye kioo au kujigusa
• Ukigundua mabadiliko yoyote, nenda kituo cha kutolea huduma za afya kilicho karibu nawe
3. Pata huduma za uchunguzi
Huduma za uchunguzi unazoweza kufanyiwa ni pamoja na kipimo cha mamogramu, kutoa ute au kinyama (biopsy) kutoka katika uvimbe
4. Zingatia mtindo bora wa maisha ili kulinda afya yako
• Zingatia uzito kulingana na ushauri wa mtaalamu wa afya
• Fanya mazoezi ya mwili mara kwa mara
• Punguza unywaji wa pombe
• Nyonyesha kwa kuzingatia ushauri wa wataalamu
• Tumia matunda na mboga mboga kila siku
• Epuka matumizi ya tumbaku
Mifano ya imani potofu zinazoenezwa mara nyingi Kuhusu Saratani ya Matiti
Uvumi: Mionzi inayotolewa kwa ajili ya tiba ya saratani ya matiti\husababisha hatari zaidi kuliko manufaa
UKWELI:
- Matibabu ya mionzi hutumika kuangamiza chembechembe za saratani.
- Lengo la matibabu ya mionzi ni kuangamiza chembechembe za saratani zilizobakia ndani au karibu na titi baada ya upasuaji.
- Matibabu ya mionzi yanaweza kusabisha athari ndogondogo ambazo huisha wiki chache baada ya kumaliza matibabu.
- Mionzi ni njia muafaka wa kutibu saratani.
Uvumi: Kama kuna historia ya saratani ya matiti katika familia, na mimi nitapata;
kama hakuna historia mimi sitapata.
UKWELI:
- Wanawake wote wako katika hatari zaidi ya kupata saratani ya matiti.
- Kuwa na ndugu mwenye Saratani ya matiti huongeza hatari ingawa si lazima upate.
- Unaweza kuwa na Saratani ya matiti hata kama huna ndugu aliyewahi kupata ugonjwa huu.
Uvumi: Saratani ya matiti mara zote huwa na uvimbe.
UKWELI:
- Mara nyingi saratani huwa na uvimbe; lakini mara nyingine saratani ya matiti hutokea bila uvimbe wowote.
- Kuna dalili nyingine 7 zinazoweza kuashiria uwepo wa saratani ya matiti
Fahamu hali ya Kawaida Kwako
Dalili za saratani ya matiti hazifanani kwa wanawake wote.
Ukigundua mabadiliko yoyote, nenda kituo cha afya kilicho
karibu nawe.
Mabadiliko ya matiti yanayopaswa
kutolewa taarifa ni pamoja na:
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni