Jumanne, 29 Oktoba 2019

Je, unataka mtoto mwenye akili darasani?, je, una wasiwasi na maendeleo ya ubongo wa mwanao?

Vyakula madhubuti kwa maendeleo ya ubongo wa mtoto!


Miaka mitatu ya kwanza katika maisha ya mtoto ni muda ambao shughuli za ubongo wa mtoto zinahitajika kwenda kwa kasi kutokana  na ugeni alionao mtoto kuhusu mazingira na vitu vinavyo mzunguka. Je, unataka mtoto mwenye akili darasani?,  je, una wasiwasi na maendeleo ya ubongo wa mwanao. Hivyobasi, Karibu sana katika makala yetu hii hususani kipengele hiki cha Lishe na Mazoezi ambapo tunapata wasaa wakukufahamisha kuhusu masuala mbalimbali yanayo husiana na lishe pamoja na mazoezi.
Leo tunakueletea elimu kuhusu vyakula ambavyo ni vya muhimu sana kwa mtoto anayeendelea kukua baada ya kuachishwa maziwa ya mama. Ifahamike kuwa, wakati wa utoto ndio kipindi pekee ambapo ubongo wa mtoto unaweza kutunzwa na hivyo kusaidia shughuli mbalimbali ambazo zitamuhitaji matumizi ya ubongo kama;

Kutunza kumbukumbu , Kutafsiri taarifa za mfumo wa fahamu , Kuelewa shuleni na kufaulu mitihani, n.k

Baadhi ya vyakula ambavyo vimefanyiwa uchunguzi na kuonekana vinasaidia katika maendeleo ya ubongo ni kama ifuatavyo;
  1. Mayai,
  2. Mboga za majani,
  3. Samaki,
  4. Maapple na matunda damu,
Mayai
Mayai ni mojawapo ya vyakula vyenye aina nyingi za virutubisho kama protini, wanga na mafuta amba vyo husaidia katika ukuaji na kuupa mwili  nguvu. Vivohivyo, mayai yanasaidia ukuaji wa ubongo wa mtoto kwakuwa yanatunza virutubisho vinavyoitwa choline na aside za mafuta yaitwayo omega-3 ambayo yanafanya kazi kubwa kipindi cha umri mdogo katika kuimarisha mpangilio wa muundo wa ubongo wa mtoto. 

Samaki
Samaki pia wanahitajika  kwa kiwango kikubwa kutokana na mchango wake katika kulinda ubongo ili usipunguze uwezo wake wa kufanya kazi na kuzuia upotevu wa kumbukumbu. Kazi hizi za ubongo husaidia watoto ambao wako katika miaka ya kwenda kusoma kuweza kuelewa na kukumbuka wanavyofundishwa darasani.

Maepple na matunda damu
Matunda haya yana kemikali iitwayo Quercetin ambayo hutumika kama dawa ya kuzuia athari za dawa nyingine zinazo haribu ubongo wa mtoto. Kemikali hii huweza ondoa sumu inayotokana na dawa hizi hivyo kusaidia ukuaji na ufanyaji kazi mzuri wa ubongo. Kemikali hii pia hupatikana katika mimea mingi kama mchaichai na mboga za majani kama sukumawiki.

Mboga za majani

Mboga za majani kama sukumawiki na spinachi, kwa kiwango kikubwa zinasaidia katika kulinda seli za ubongo na kusidia ukuajia wenye afya.


Kwa namna moja ama nyingine wazazi wenye watoto wanatamani watoto wao wawe wenye akili na wanaojielewa na wenye kuyaelewa mazingira na vitu vinavyowazunguka kwa urahisi. Vyakula tajwa ni muhimu sana kwa mtoto ambaye amekwisha achishwa maziwa ya mama ili kumsaidia katika ukuaji ubongo na mwili kwa ujumla.

Alhamisi, 24 Oktoba 2019

Ujumbe kuhusu kinga na tiba ya saratani ya matiti


1. Fahamu visababishi 
• Kurithi
• Umri mkubwa 
• Kupata mtoto wa kwanza baada ya umri wa miaka 35 
• Uzito mkubwa 
• Kutokufanya mazoezi 
• Matumizi ya tumbaku au pombe

2. Fahamu hali ya kawaida kwako

• Fahamu hali ya kawaida ya matiti yako kwa kujitazama kwenye kioo au kujigusa 
• Ukigundua mabadiliko yoyote, nenda kituo cha kutolea huduma za afya kilicho karibu nawe

3. Pata huduma za uchunguzi 

Huduma za uchunguzi unazoweza kufanyiwa ni pamoja na kipimo cha mamogramu, kutoa ute au kinyama (biopsy) kutoka katika uvimbe

4. Zingatia mtindo bora wa maisha ili kulinda afya yako

• Zingatia uzito kulingana na ushauri wa mtaalamu wa afya 
• Fanya mazoezi ya mwili mara kwa mara 
• Punguza unywaji wa pombe 
• Nyonyesha kwa kuzingatia ushauri wa wataalamu 
• Tumia matunda na mboga mboga kila siku 
• Epuka matumizi ya tumbaku

Mifano ya imani potofu zinazoenezwa mara nyingi Kuhusu Saratani ya Matiti

Uvumi: Mionzi inayotolewa kwa ajili ya tiba ya saratani ya matiti\husababisha hatari zaidi kuliko manufaa
UKWELI: 
  • Matibabu ya mionzi hutumika kuangamiza chembechembe za saratani.
  • Lengo la matibabu ya mionzi ni kuangamiza chembechembe za saratani zilizobakia ndani au karibu na titi baada ya upasuaji. 
  • Matibabu ya mionzi yanaweza kusabisha athari ndogondogo ambazo huisha wiki chache baada ya kumaliza matibabu. 
  • Mionzi ni njia muafaka wa kutibu saratani.
Uvumi: Kama kuna historia ya saratani ya matiti katika familia, na mimi nitapata; kama hakuna historia mimi sitapata.
UKWELI: 
  • Wanawake wote wako katika hatari zaidi ya kupata saratani ya matiti.
  •  Kuwa na ndugu mwenye Saratani ya matiti huongeza hatari ingawa si lazima upate.
  • Unaweza kuwa na Saratani ya matiti hata kama huna ndugu aliyewahi kupata ugonjwa huu. 
Uvumi: Saratani ya matiti mara zote huwa na uvimbe. 
UKWELI:
  • Mara nyingi saratani huwa na uvimbe; lakini mara nyingine saratani ya matiti hutokea bila uvimbe wowote.
  • Kuna dalili nyingine 7 zinazoweza kuashiria uwepo wa saratani ya matiti
Fahamu hali ya Kawaida Kwako
Dalili za saratani ya matiti hazifanani kwa wanawake wote. Ukigundua mabadiliko yoyote, nenda kituo cha afya kilicho karibu nawe.

Mabadiliko ya matiti yanayopaswa kutolewa taarifa ni pamoja na:





Alhamisi, 17 Oktoba 2019

Female Afya+

Uvutaji sigara, vyakula tunavyokula na vinywaji tunavyokula hubadili rangi ya meno yetu meupe. Pia vile mtu anavyozeeka ndivyo rangi ya meno hufubaa. Bofya https://buff.ly/2FIswAX kujua siri 10 za kuwa na meno yanayong'aa.

Image may contain: 1 person, smiling

Female Afya+

Faida za kuhudhuria kliniki: Kutia hamasa na kuimarisha afya ya mwili, akili na jamii ya mama kwa kutoa elimu juu ya lishe, usafi, kupumzika n.k. Kutambua na kutibu mapema matatizo ya afya ya mama na kasoro za maumbile. Pia kuunganishwa na elimu kwa simu.

Image may contain: 1 person, smiling, sitting and phone

Female Afya+

Kadiri mwanamke anavyofahamu mambo mengi zaidi kuhusu mimba yake tangu tu anapohisi kuwa mjamzito ndivyo alivyo na nafasi nzuri ya kufanikiwa kujifungua kwa usalama
Image may contain: 2 people, people smiling, indoor

Female Afya+

Maumivu ya hedhi husababishwa na kukakamaa kwa misuli ndani ya mfuko wa uzazi inayopelekea mishipa ya damu kukandamizwa. Mishipa ya damu ikikandamizwa hushindwa kupeleka damu yenye oksijeni. Ukosefu wa oksijeni kwenye misuli hiyo huleta maumivu makali.

Image result for maumivu ya hedhi

Jumatatu, 7 Oktoba 2019

Ni kweli Maziwa ya ng’ombe yanaponyesha vidonda vya tumbo?

Image result for peptic ulcer disease symptoms

Ni kweli Maziwa ya ng’ombe yanaponyesha vidonda vya tumbo?

Kinyume na dhana iliyozoeleka ndani ya jamii, maziwa ya ng'ombe hayaponyeshi vidonda vya tumbo, bali huongeza madhara yatokanayo na ugonjwa huu. Hii ni kwa sababu, maziwa huwa na tabia ya kutengeneza aina fulani ya kinga au ukuta (protective coat) kwa vimelea vya Helicobacter Pylori ambayo huvikinga vimelea hivi dhidi ya mashambulizi ya dawa na hivyo kufanya dawa kushindwa kuwaua na kuwaondoa kabisa vimelea hivi.
Kinachotokea ni kuwa, maziwa huondoa tu kwa muda maumivu ya tumbo kwa kupunguza makali ya tindikali iliyopo tumboni. Pindi maziwa haya yanapoisha, maumivu hurejea tena na kuwa makali kama hapo awali.