Ijumaa, 27 Septemba 2019

Mambo 5 unayotakiwa kujua kuhusiana na hedhi

Image result for hedhi
Je unafahamu inakadiriwa kuwa, mwanamke hupata hedhi wastani wa mara 400 katika maisha yake? Pia, neno linalotumika sana kuwakilisha hedhi ni "period", neno hili lilianza kutumika kwa mara ya kwanza kwenye miaka ya 1822 likimaanisha tukio linalotokea ndani ya muda fulani au linalojirudia baada ya muda fulani. Leo hii tuangalie mambo mengine 5 muhimu kuyajua kuhusiana na hedhi.
1. Kwa wastani, mwanamke huanza kupata hedhi yake ya kwanza kabisa akiwa na umri wa miaka 12.
2. Mzunguko wa siku za hedhi huwa kati ya siku 21 hadi 35. Ingawa wengi huwa na mzunguko wa siku 28, lakini kuzidi wiki moja au kuwahi kwa wiki moja ni kitu cha kawaida.
3. Mwanamke huzaliwa na mayai milioni 1 hadi 2. Mayai haya, mengi hufa jinsi mwanamke anavyoendelea kuishi na ni mayai 400 tu ndiyo hukadiriwa kufika hatua ya ukomavu tayari kwa uchavushwaji.
4. Msichana anaweza kupata ujauzito kabla ya kuanza hedhi yake ya kwanza. Hii ni kwa sababu, yai huanza kukomaa kabla ya kuona hedhi yake ya kwanza, hivyo kama atashiriki tendo bila kinga, kuna uwezekano wa kupata ujauzito.
5. Wanawake wengi hufikia ukomo wa kupoata hedhi (menopause) wakiwa na umri wa miaka 48 hadi 55.

Dalili, tiba na kinga ya ugonjwa wa UTI

Dalili, tiba na kinga ya ugonjwa wa UTI
Maambukizi ya njia ya mkojo (UTI) husababishwa na vimelea kitaalamu hujulikana E. Coli. Vimelea hawa huishi huishi kwenye mfumo wa chakula bila kuleta madhara yoyote wawapo humo, ila wakiingia kwenye njia ya mkojo huleta maambukizi n kusababishwa ugonjwa wa UTI.
Kutokana na sababu za kimaumbile, Wanawake huathirika zaidi na ugonjwa wa UTI kuliko wanamume, hii ni kwa kwasababu kuna ukaribu zaidi katika njia hizi mbili za chakula na mkojo. Na pale mtu anaponawa baada ya haja kubwa ni rahisi zaidi kuhamisha vimelea hivi vya E. Coli  kwenye njia ya mkojo pale ambapo hujifuta kuelekea mbele.  Na ndiyo sababu, kwa wanawake, hushauriwa kunawa kuanzia mbele kuja nyuma. Endapo utanawa kuanzia nyuma kuja mbele, kuna uwezekano wa kuhamisha vimelea hivi ambavyo husambaa hadi kwenye kibofu, na endapo hautotibiwa vyema, basi hupanda hadi kwenye figo.
Pia, Wanawake huathiriwa sana na UTI kwa sababu wana njia nyembamba ya mirija ya mkojo (urethra) ambayo, inawapa bakteria wa UTI urahisi wa kusafiri hadi kwenye kibofu cha mkojo. Kujamiiana pia kunaweza kunaweza kupelekea kupata bakteria wanaosababisha UTI.

Dalili za maambukizi ya njia ya mkojo

  • Maumivu wakati wa haja ndogo, na hisia ya mkojo kuchoma choma
  • Kubanwa na mkojo mara kwa mara
  • Maumivu ya kiuno na maumivu ya chini ya kitovu
  • Mkojo wa njano sana, na muda mwingine unatoa harufu
  • Uchovu
  • Homa
  • Kuna baadhi ya watu hawawi na dalili yoyote (asymptomatic bacteriuria)
  • Kichefuchefu na kutapika
Unapohisi dalili hizi ni vyema kwenda kwa daktari ili upate tiba muafaka badala ya kuanza kutumia madawa bila ya mpangilio maalumu kitu kitakachoweza kukusababishia kukomaza ugonjwa. Pia, kuna baadhi ya dalili za UTI hufanana na zile za magonjwa ya zinaa (chlamydia, gonorrhea, and trichomoniasis), hivyo, vipimo vya maabara huitajika kuweza kutambua kama unachoumwa ni UTI au ni magonjwa ya zinaa (STD)

Vipimo:

  • Kupima mkojo kuangalia kama kuna chembe chembe nyeupe,na vimelea ambacho ni kiashirio cha maambukizi
  • Kuotesha mkojo kuangalia vimelea
  • Ultrasound ya tumbo chini ya kitovu kuangalia njia ya mkojo na hasa kibofu

Jinsi ya kujikinga na maambukizi ya njia ya mkojo

  • Kunywa maji mengi
  • Baada ya haja kubwa ni vizuri kunawa kuanzia mbele kurudi nyuma
  • Pendelea kwenye kukojoa pindi unapojisikia umeshikwa na mkojo. Na hakikisha umetoa mkojo wote.
  • Hakikisha sehemu za siri zipo safi kabla ya kujamiia
  • Ni vizuri kupata haja ndogo mara baada ya kujamiana ili kusafisha bakteria ambao wanaweza kuwepo kwenye njia ya mkojo,
  • Tumia juisi ya Cranberry ina vitu kitaalamu Vitamins and antioxidants ambavyo husaidia kuzia (siyo kutibu) maambukizi haya.
  • Hakikisha sehemu za siri zipo kavu, pendelea kuvaa nguo za ndani zilizotengenezwa kwa pamba, pia zenye kuacha unafasi (loose-fitting), epuka jinsi zinazobana au nguo za ndani za unailoni kwa sababu zitapelekea kuwa na hali ya unyevunyevu na kuleta mazingira rafiki kwa ukuaji wa bakteria.

UTI kwa wajawazito

Anawake wajawazito wapo kwenye hatari kupatwa na ugonjwa wa UTI. Homoni wakati wa ujauzito hupelekea kutokea mabadiliko kwenye nia ya mkojo. Pia, uterus huongeza mgandamizo kwenye mishipa inayopitisha mkojo kutoka kwenye kibofu (ureter) na kibofu chenyewe, hali hii husababisha mkojo kupita kwa shida kutoka kwenye figo kuja kwnye kibofu au kutoka kwenye kibofu chenyewe. UTI isiyotibiwa huweza kuleta athari kwa ikiwemo preterm labor.

UTI kwa watoto wadogo

Watoto wadogo, pia wanaweza kupata ugonjwa wa UTI ingawa mara nyingi ni ngumu kwa mzazi kutambua kwa sababu ni ngumu kujieleza. Mara nyingi unaweza kuona dalili zifuatazo
  • Homa
  • Harufu tofauti ya mojo
  • Kukataa vyakula au kutapika
  • Kusumbuasumbua (Fussy behaviour)
Unashauriwa kumpelekea hospitali kwa ajili ya matibabu punde unapohisi ana UIT ili kuzuia athari Zaidi. Pia, kubadilisha nepi kunasaidia kupunguza uwezekano wa maambukizi. Kumbuka, kumsafisha kutokea mbele kuja nyuma wakati unambadilisha nepi na kumsafisha.

Hatari za UTI

Hatari kubwa ya kukaa na UTI ni kuwa, bakteria wanaweza kusambaa hadi kutoka kwenye kibofu hadi kwenye figo. Bakteria hawa huweza kuathiri ufanyaji kazi wa figo kitu ambacho ni cha hatari haswa kwa watu wenye matatizo ya figo. Pia, kuna uwezekano mdogo wa bakteria hawa kuingia kwenye mfumo wa damu, endapo hatua hii itatokea, basi huweza kusababisha kuthirika kwa viungo vingine. Hatari kwa mama mjamzito kupata maambukizi ya njia ya mkojo huweza kupelekea kujifungua kabla ya wakati, au kujifungua mtoto mwenye uzito mdogo.
Kama una maswali kuhusiana na ugonjwa wa UTI, usisite kuacha maoni hapo chini.

KUYAFANYA MENO YENYE RANGI KUWA MEUPE

Kuyafanya Meno Yenye Rangi kuwa Meupe (Teeth Whitening)
Wakati wa muongo uliopita mahitaji ya kuboresha muonekano au kurembesha meno yameongezeka kwa kiwango kikubwa hasa katika nchi zilizoendelea. Hii imechochewa na kupatikana kemikali mpya za meno (dental meterials) na vifaa kwa kasi ikiendana na kuboresha vile vya zamani. Sehemu nyingine iliyosababisha madaktari na mainjinia wa meno kuyafanya meno kuwa meupe ni sehemu ya fani ya taaluma ya meno chini ya urembeshaji wa meno, fani hii uhusika na kuboresha muonekano wa meno hasa yale yanayoonekana wakati wa kutabasamu na kuongea.
Inahusisha matibabu kama kuyafanya meno yenye rangi kuwa meupe, kunyoosha meno yaliyojipanga vibaya pamoja na kukarabati meno yaliyovunjika na yale yaliyoumbika visivyo (malformed teeth). Huko Uingereza na sehemu nyingine za magharibi wanawake walio wengi wanatumia maelfu ya paundi/euro kuboresha muonekano wa meno yao hali ambayo inaanza pia kuingia huku kwetu.
Nini husababisha meno kugeuka rangi?
Meno kugeuka rangi husababishwa na kimojwapo au muunganiko wa vitu vifutavyo: -
  1. Vyakula na vinywaji kama vile vinyaji vyenye kaboni, wine na sigara.
  2. Utumiaji wa maji yenye kiwango cha juu cha madini aina ya magadi (fluoride) na utumiaji wa magadi katika kulainisha vyakula wakati wa kuandaa vyakula vigumu kama maharage na makande. Utafiti uliofanywa na Prof. Mabelya na wenzake nchini Tanzania umeonesha kuwa kubadilika kwa rangi ya meno kutokana na magadi kwa kiwango kikubwa husababishwa na matumizi ya magadi katika mapishi ya vyakula hasa makande kule maeneo ya mkoa wa Kilimanjaro/Moshi kuliko inavosababishwa na matumizi ya maji.
  3. Maumbile yasiyo sahihi ya sehemu ngumu za jino (enamel and dentine defects). Iwapo sehemu ngumu ya meno imeumbwa ikiwa laini ni rahisi kufyonza rangi na jino kuota likiwa limegeuka rangi au kubadilika baada ya kuota.
  4. Matumizi ya madawa kwa mama mjamzito ambaye tayari meno ya mtoto aliye tumboni yameanza kuumbwa lakini hayajapata madini ya kutosha na hata watoto wachanga ambao meno yao hayajakomaa.
  5. Kufa kwa kiini cha jino hasa kutoka na kujigonga wakati wa ajali au kupigana ngumi usoni (pulp necrosis), jino likigongwa kwa nguvu damu huvuja ndani ya kiini cha jino na baadaye huchachuliwa na kutoa kemikali ambayo hupenya kwenye vitundu vidogo vidogo kwenye dentine na kujidhihirisha kama kijivu, zambarau au hata nyeusi. Hali hii yaweza tokea mapema baada ya kupata ajali lakini wakati mwingine inaweza kuchukua miaka kadhaa hata arobaini kipindi ambapo mtu hakumbuki kuwa aliwahi kutwangwa ngumi.
Kuyafanya meno yenye rangi yasimpendeza mwenye nayo kuwa meupe (Bleaching or teeth whitening)
Huku ni kuyafanya meno yenye rangi kuwa meupe au kuongeza weupe wa yale yenye rangi ya kawaida kufikia kiwango cha weupe atakacho muhitaji kwa kutumia kemikali maalum. Rangi ya kawaida ya meno kwa walio wengi ni uweupe kama wa maziwa (milky white). Rangi yeyote nje ya hiyo si ya kawaida (abnormal color or discoloration).
Kuwa na rangi isiyo ya kwaida hasa kwa meno ya mbele linaweza kuwa tatizo kubwa la urembo na kumsumbua mhusika kisaikolojia. Kuyafanya meno kuwa meupe kumelenga kuwaondolea wahusika tatizo hili japo mafanikio yake yanategemea kiwango cha rangi isiyo ya kawaida.
Kufanya meno kuwa meupe kwa kutumia kemikali, kunaweza kubadili yaliyo na rangi isiyo ya kawaida kutoka yale yaliyoathirika kwa kiwango kidogo mpaka cha kati. 
Kufanya meno yawe meupe kwa kutumia kemikali huunguza (oxidises) rangi ya jino na kuiondoa. Kemikali zinazotumika   zina hydrogen peroxide 30%-35% na baadhi carbamide peroxide 10%. Kemikali hizi huweza kuondoa rangi zilizosababishwa na vyakula, vinywaji, dawa za tetracycline, rangi kidogo iliyotokana na utumiaji wa madini ya magadi kwenye vyakula au kwenye maji (mild fluorosis) na meno yenye rangi ya njano au kijivu itokanayo na umri kuwa mkubwa. Inaweza pia kuondoa rangi itokanayo na uvutaji wa sigara na matumizi ya ugoro.
Kwa wavutaji wa sigara sharti waache pindi watumiapo kemikali hizi kwani muunganiko wa hydrogen peroxide na kemikali zilizopo kwenye moshi wa sigara unahisiwa kuongeza madhara zaidi ambayo tayari moshi wa sigara husababisha kwenye mwili wa binadamu. Haishauriwi kwa akina mama wanaonyonyesha kutumia dawa hizi pamoja na kwamba hakuna madhara yanayojulikana mpaka sasa. 


Kuboresha weupe kwa kutumia chemikali

Kupiga meno viraka (Veneering)
Hii hufanyika kwa kuondoa sehemu ndogo ya juu ya jino kwenye enamel kama 0.5-1mm na baadaye kupandika dawa yenye rangi nyeupe kulingana na mgonjwa anavyotaka mwenyewe. Picha inayonesha meno yaliyobadlika rangi kutokana na magadi kabla na baada ya kupigwa viraka
 
Kabla ya kiraka                                                        Baada ya kupigwa kiraka (veneer)
Kumbuka: kuna rangi zaidi ya 26 nyeupe ambazo miongoni mwake mgonjwa anaweza kuchagua anayoitaka

Maambukizi ya Fangasi katika Sehemu za Siri

Maambukizi ya Fangasi katika Sehemu za Siri (Vaginal Candidiasis)

Maambukizi ya Fangasi katika Sehemu za Siri (Vaginal Candidiasis)

Kati ya maambukizi yanayowasumbua wanawake wengi duniani ni maambukizi ya fangasi. Inakisiwa asilimia 75 ya wanawake wote duniani hupata maambukizi haya katika kipindi cha uhai wao. 
Maambukizi ya fangasi katika sehemu za siri za mwanamke husababishwa na uwepo wa fangasi wanaojulikana kitaalamu kama Candida albicans. Maambukizi haya pia hujulikana kama yeast infection au thrush. Fangasi hupatikana kama vimelea vya kawaida katika mdomo, mpira wa kupitisha chakula sehemu inayojulikana kama pharynx, katika kibofu cha mkojo, uume na hata kwenye uke. 
Mfumo mzuri wa kinga wa mwili pamoja aina fulani za bakteria wanaoishi pamoja na fangasi hawa husaidia sana katika kuthibiti maambukizi yanayoyosababishwa na aina hi ya fangasi. 

Nini hutokea?

Kwa kawaida, Candida albicans huishi kwenye uke na sehemu nyingine (kama zilivyoelezewa hapo juu) bila kusababisha madhara yoyote yale isipokuwa pale mazingira ya eneo husika yanapobadilika kama vile mabadiliko katika hali ya pH ya  eneo husika (ifahamike ya kwamba pH ya kawaida ndani ya  uke ni 4.0 - 4.5) au uwiano wake na vimelea  (microorganisms) wengine unapoharibiwa kutokana na sababu mbalimbali kama vile matumizi ya madawa aina ya antibiotics, kupungua kwa kinga mwilini kutokana na magonjwa mbalimbali n.k.
Maambukizi haya ya fangasi yanaweza kugawanywa katika sehemu kuu mbili
  • Maambukizi yasiyo makali yaani uncomplicated thrush: Katika kundi hili, mgonjwa hupatwa na maambukizi  mara moja hadi nne kwa mwaka na dalili zake huwa si mbaya sana na maambukizi haya husababishwa na fangasi wa jamii hii ya Candida albicans.
  • Maambukizi makali yaani complicated thrush: Katika kundi hili, mgonjwa hupatwa na maambukizi zaidi ya mara nne kwa mwaka, dalili zake kuwa mbaya zaidi au kama maambukizi  yatakuwa yametokea kipindi cha ujauzito, ugonjwa wa kisukari, upungufu wa kinga mwilini. Aina hii kusababishwa na vimelea vya aina nyingine tofauti na Candida albicans. 

Vihatarishi

Watu walio katika hatari ya kupata maambukizi ya fangasi hawa ni  wale wenye
• Kutumia sana dawa aina ya detergents kwenye sehemu za siri au douches (vifaa vinavyotumiwa kusafishia uke kwa kutumia maji yaliyochanganywa na siki au antiseptic yoyote ile) kwa sababu hali husababisha kuharibika kwa uwiano wa fangasi na aina nyingine ya vinyemelezi kama bakteria aina ya lactobacilli
• Kutumia sana madawa aina ya antibiotics, steroids ambayo yana tabia ya kushusha kinga ya mwili
• Mabadiliko ya mfumo wa homoni mwilini ambayo husababisha mabadiliko katika s ehemu za siri na hivyo kufanya kuwepo kwa ukuaji wa kasi wa fangasi hawa
• Ujauzito (kutokana na kubadilika kwa mfumo wa homoni mwilini na kupungua kwa kinga ya mwili). Hata hivyo ieleweke hapa kuwa si kila mjamzito hupatwa na maambukizi haya.
• Matumizi ya dawa za kupanga uzazi (vidonge vya majira)
• Upungufu wa kinga mwilini kutokana na magonjwa sugu kama kisukari, saratani aina yoyote ile, ugonjwa aina ya mononucleosis na nk. 
• Ugonjwa wa ukimwi (HIV/AIDS)
• Matibabu ya homoni (hormonal replacement therapy) kutokana na sababu mbalimbali
• Matibabu ya kusaidia kushika mimba kwa wale wenye matatizo ya uzazi (infertility treatment)
• Msongo wa mawazo (stress)
• Utapia mlo (malnutrition)
• Kuvaa nguo au mavazi yanayoleta joto sana sehemu za siri kwa muda mrefu kama nguo za kuogelea (swimwear), nguo za ndani (chupi)  zilizotengenezwa kwa kitambaa aina ya nylon, nguo za ndani zinazobana sana nk.
• Kujamiana kwa njia ya kawaida mara tu baada ya kujamiana  kupitia njia ya haja kubwa (anal sex) au matumizi ya vilainishi venye glycerin wakati wa kujamiana pia yamehusishwa na maambukizi haya.
• Kuvimba kwa tezi la koo (goiter)
• Saratani ya tezi la koo (thyroid cancer)
• Wanawake wenye umri wa miaka kati ya ishirini na thelathini wapo kwenye hatari kubwa ya kupata maambukizi haya wakati wale ambao wameshaacha kupata hedhi au wale ambao hawajaanza kupata hedhi kabisa hawako kwenye hatari kubwa. 
Kwa wanaume vihatarishi  vya maambukizi haya ni
• Kujamiana na mwanamke mwenye tatizo hili au maambukizi haya
• Upungufu wa kinga mwilini
• Matumizi ya madawa aina ya antibiotics kwa muda mrefu bila ushauri wa daktari
• Magonjwa sugu kama kisukari, saratani ya aina yoyote ile na nk.
Dalili na viashiria kwa wanawake
• Kuwashwa  sehemu za siri  (kwenye tupu ya mwanamke)
• Kuhisi kuwaka moto sehemu za siri (burning sensation)
• Kufanya kama vidonda katika sehemu za siri (soreness)
• Maumivu wakati wa kujamiana (superficial dyspareunia)
• Maumivu  au usumbufu wakati wa kujisaidia haja ndogo (wakati mtu anakojoa)
• Kuvimba na kuwa rangi nyekundu kwa  mdomo wa nje wa tupu ya mwanamke (labia minora)
• Kutokwa na uchafu wa rangi nyeupe au nyeupe kijivu, unaoweza kuwa mwepesi, majimaji au mzito na ambao umefanana na jibini (cottage cheese like discharge) wenye muonekano unaojulikana pia kama curd-like appearance. Kwa kawaida, uchafu huu haumbatani na harufu yoyote isipokuwa panapokuwa na tatizo la ziada kama ugonjwa wa zinaa aina ya Bacteria vaginosis. Uchafu huu unaotoka hapa unaweza kuenea kwenye maeneo mengine yaliyokaribu na tupu ya mwanamke kama kwenye mitoki (groin area) au perineum na kusababisha kuharibika kwa ngozi katika sehemu hizo.
Dalili na viashiria hivi huwa mbaya zaidi wakati  mwanamke anapokaribia  kupata hedhi. 
Dalili na viashiria kwa wanaume ni
• Kuwashwa sehemu za siri  
• Kuvimba na kuwa rangi nyekundu kwenye ncha ya uume
• Kuwepo kwa uchafu wa rangi nyeupe (kama nilivyoeleza hapo juu) kwenye sehemu ya juu ya uume.
• Kuwa na vidonda vidogo kwenye uume (sore on the glans) 
Hata hivyo, mara nyingi wanaume hawaoneshi dalili zozote zile, ni vizuri kwa mwanamke kumueleza mwenza wake pale anapopata maambukizi haya ili naye pia apate kutibiwa. 

Vipimo vya uchunguzi

Kabla ya vipimo vya uchunguzi, ni muhimu kwa daktari kuchukua historia ya mgonjwa kwa usahihi kabisa. Vipimo vitahusisha:

Uchunguzi wa uke (per Vaginal Examination (PV exam)

Daktari huvaa gloves, na kuzilainisha gloves hizi kwa jelly maalum, mgonjwa hulala kwenye kitanda na kutanua miguu yake ili njia itanuke na kumrahisishia daktari kumfanyia uchunguzi, wakati  akiwa tayari, daktari ataingiza vidole vyake viwili (cha shahada na cha kati) ukeni kwa dhumuni la
  • Kuhisi kama kuna uvimbe wowote ndani ya tupu ya mwanamke 
  • Kuangalia kama anapata maumivu wakati wa kujamiana
  • Kuangalia kama kuna uchafu wowote unaotoka, wingi wake, rangi yake, harufu yake, uzito wake (mwepesi, majimaji au mzito), na aina ya uchafu unaotoka kama ni sahihi kutokana na maelezo ya mgonjwa au ni tofauti
  • Kuangalia kama sehemu ya siri ipo kawaida
  • Kuangalia kama kuna uvimbe wowote wa tezi za sehemu ya siri (mitoki)
  • Kuangalia nywele za sehemu za siri zilivyo na jinsi zilivyokaa
  • Kuangalia shingo ya kizazi, bartholin glands nk.
  • Kuangalia sehemu ya haja kubwa kama kuna skin tags, bawasiri (haemorrhoids) nk.
  • Kuangalia kwenye kinembe (clitoris) kama kuna tatizo lolote lile. 
Hayo ni baadhi tu ya malengo na faida za kipimo hiki kwa vile humuwezesha daktari kugundua tatizo au maradhi mengine ya ziada ambayo hayajaanza bado kuonesha dalili zake kwa mgonjwa au mgonjwa mwenyewe hafahamu kama hali aliyo nayo ni tatizo. Hata hivyo inashauriwa sana kabla ya kufanya kipimo hiki, daktari amjulishe mgonjwa aina ya kipimo, lengo lake na jinsi kitakavyofanyika ili kumuandaa mgonjwa kisaikolojia. Aidha ni muhimu pia kumtaarifu wakati anapoanza kuingiza vidole.
Kuchunguza uchafu unaotoka kwa kutumia hadubini (microscope).
Mara tu baada ya kuchukua sehemu ya uchafu kwa kutumia swab, kipimo hicho humwagiwa tone la 10% potassium hydroxide ambayo huyeyusha chembechembe za ngozi na kubakisha seli za Candida albicans. Kuwepo kwa pseudohyphae (mfano wa aina fulani ya mizizi au miguu ya fangasi hawa) pamoja na budding yeast cells (yaani seli za fangasi zinazojigawa kwa ajili ya kuzaliana) ni uthibitisho wa maambukizi ya fangasi aina ya Candida albicans.
Kuchukua kipimo na kuotesha kwenye maabara
ili kuangalia aina ya uoto huo kama ni wa fangasi aina ya Candida albicans, ama la.
Kipimo cha mkojo (Urinalysis)
Vipimo vingine hufanyika kulingana na dalili zinazoashiria uwepo wa magonjwa mengine kama vile ugonjwa wa kisukari, HIV/AIDS, ugonjwa wa  kuvimba tezi la koo (goiter), saratani ya tezi koo (thyroid cancer) nk.

Matibabu

Matibabu ya fangasi huusisha dawa za kutibu fangasi (antifungal drugs) kama vile dawa za kupaka za topical Clotrimazole, topical Nystatin, Fluconazole au topical Ketoconazole.  
Wagonjwa wenye maambukizi yasiyo makali yaani uncomplicated vaginal candidiasis wanaweza kutumia dawa za kupaka (cream) kutoka dawa za fangasi za jamii ya -azole kama vile Butoconozale, Miconazole, Clotricomazole nk. Dawa hizi hutumika kwa muda wa siku 3-7 kulingana na aina ya dawa. Mgonjwa anashauriwa kupaka dawa ndani ya uke pamoja na maeneo yote yanayozunguka sehemu hiyo. Jinsi ya kupaka dawa hizi ni kuanzia mbele kuelekea nyuma. 
Aidha mgonjwa anaweza kupewa dawa za kutumbukiza ukeni ambayo atatumia kwa muda wa siku 3-14 kulingana na aina ya dawa. Dawa hizo ni pamoja na Miconazole, Tiaconazole, Terconazole, Nystatin nk.
Kidonge cha kumeza aina ya fluconzole pia huweza kutolewa. Dawa hizi nilizotaja hapa juu zina kawaida ya kuharibu ubora wa mipira ya kondomu zilizotengenezwa na mpira aina ya latex (latex condoms) pamoja na vifaa vya upangaji uzazi aina ya diaphragms.
Ni vizuri kwa daktari kabla ya kumpa mgonjwa dawa hizi kumfahamisha kwa ufasaha jinsi ya kuzitumia na tahadhari anayotakiwa mgonjwa kuchukua. Inashauriwa kama baada ya matumizi haya bado mgonjwa ana dalili za maambukizi au mgonjwa akapata tena maambukizi haya ndani ya miezi miwili baada ya matibabu ya awali, basi anashauriwa kwenda kumuona daktari ili apate matibabu zaidi.
Kwa wale wenye maambukizi makali yaani complicated vaginal candidiasis, kabla ya kupewa tiba, ni muhimu kwanza kufanyiwa kipimo cha kuotesha sehemu ya uchafu unaootoka ukeni ili kuwa na uhakika kama kweli fangasi wanaosababisha maambukizi haya ni Candida albicans ama la, kwani fangasi aina ya Candida glabrata pia wanaweza kusababisha aina ya maambukizi haya na huwa siyo rahisi kutibika kwa kutumia matibabu ya kawaida ya kutibu fangasi pamoja  na pia si rahisi kuonekana kwa kutumia hadubini (microscope).
Matibabu ya wagonjwa wenye aina hii ya fangasi hujumuisha matumizi ya dawa za kupaka au vidonge vya kuweka ukeni kwa muda mrefu yaani kwa muda wa siku saba hadi kumi na nne (7-14) au dawa aina ya fluconazole ambayo hutumika kila baada ya siku tatu (yaani siku ya 1, siku ya 4 na siku ya 7).
Mara baada ya kumaliza tiba hii, mgonjwa hutakiwa kuendelea nayo mara moja kwa wiki kwa muda wa miezi sita. Ikiwa matibabu haya hayatasaidia basi mgonjwa anaweza kushauriwa kutumia mchanganyiko wa fluconazole pamoja na dawa ya kupaka ya Clotrimazole mara mbili au moja kwa wiki kulingana na dozi ya dawa, au fluconazole na dawa nyingine za kupaka kwa wakati mmoja. 
Matibabu ya wagonjwa wenye maambukizi hatari sana yaani severe vaginal candidiasis ambayo kwa kawaida huambatana na dalili kama uke kuwa mwekundu sana, uke kuvimba, michubuko ya ngozi ya ukeni (excoriation) na kutokea kwa mifereji kama vidonda (fissure formation) huwa ni dawa zozote za kupaka zilizotajwa hapo juu kwa muda wa siku 7 mpaka 14 au dawa ya fluconazole ambayo hutolewa mara mbili, ambapo dozi ya pili hutolewa siku ya tatu baada ya kutolewa kwa dozi ya awali (second dose 72hrs after initial dose).
Matibabu ya maambukizi ya fangasi ambayo hayasababishwi na Candida albicans kwa mfano Candida glabrata nk ni matumizi ya dawa za kupaka jamii ya nonfluconazole azole groups kama vile Posaconazole, Voriconazole nk zitolewazo kwa muda wa siku 7 mpaka 14 pamoja na kidonge cha Boric acid kwa muda wa siku 14. Mtu mwenye maambukizi haya pia anashauriwa kuonana na daktari bingwa wa magonjwa ya akina mama. 
Kwa vile maambukizi ya fangasi hutokea sana kwa wanawake wajawazito, hivyo basi wanashauriwa kutibiwa kwa kutumia dawa za kupaka tu kwa muda wa siku 7.
Aidha dawa aina ya Itraconazole haipaswi kutumiwa na mwanamke mjazito au anayekusudia kushika mimba. Dawa ya Ketoconazole haipaswi kutolewa bila ushauri wa daktari kwani ina madhara ya kusababisha ugonjwa hatari wa Ini (Fulminant hepatitis). Usugu wa fangasi dhidi ya dawa za jamii ya azole groups hutokea baada ya matumizi ya  dawa za  vidonge (vya kumeza) za kutibu  fangasi  kwa muda mrefu. 
Maambukizi ya fangasi pia huonekana sana kwa wagonjwa wenye Ukimwi. Tiba ya maambukizi haya ni sawa na tiba ya watu ambao hawana ugonjwa wa Ukimwi. Hata hivyo, kwa wale wagonjwa wa ukimwi ambao wamepata maambukizi ya fangasi mara kwa mara wanashauriwa kunywa dawa aina ya fluconzole mara moja kwa wiki kama kinga dhidi ya maambukizi haya au kama njia ya kupunguza fangasi hawa.
Kadhalika dawa za kutibu fangasi aina ya Itraconazole, Voriconazole, Posaconazole huingiliana sana katika utendaji kazi na dawa za kurefusha maisha za ugonjwa wa Ukimwi (Antiretroviral drugs, ARVs) aina ya Protease Inhibitors, PIs (rotinavir nk.) na Nonnucleoside Reverse Trancriptase Inhibitors, NNRTI (maraviroc nk). 
Wakati mwingine, maambukizi ya fangasi yanaweza kuambatana na magonjwa ya zinaa (Bacterial vaginosis nk), hivyo dawa zitatolewa kulingana na dalili na historia ya mgonjwa. 

Kinga ya maambukizi ya fangasi

• Kuosha sehemu ya siri kwa kutumia kitambaa kisafi kila siku na kuosha kuanzia mbele kuelekea nyuma, epuka kurudia ukishafika nyuma.
• Epuka matumizi ya sabuni zenye manukato, bubble baths, vaginal deodorant products, feminine hygiene, na bath powder.
• Vaa chupi ambazo hazibani sana na zilizotengenezwa kwa kutumia pamba au hariri (silk), epuka synthetic underwear.
• Epuka mavazi yoyote ya kubana kama jeans za kubana nk.
• Badilisha nguo za ndani (chupi) kila zinapopata unyevunyevu.
• Fua chupi zako kwa maji yenye nyuzi joto 90 na kuendelea.
• Tumia pad wakati tu unapozihitaji (kama umeingia kwenye mzunguko wako wa hedhi)
• Kula mlo wenye virutubisho vyote kamili (balanced diet)
• Epuka kufanya mapenzi  na mpenzi wako ambaye amepata maambukizi ya fangasi.
• Epuka kuoga  maji moto sana (hot baths) tumia maji ya uvuguvugu, hii kwa wale ambao wanaishi kwenye ukanda wa joto (tropical climate).
• Matumizi ya vifaa vya ngono (sex toys), vifaa vya upangaji uzazi (diaphragms, cervical caps) yanaweza kuleta kujirudia kwa maambukizi ya fangasi kama havitaoshwa  na kukaushwa vizuri baada ya kutumiwa.
• Baadhi ya tafiti zilizofanyika, zimethibitisha ya kwamba unywaji wa maziwa ya mtindi (yoghurt) yenye live culture, husaidia kupunguza maambukizi ya fangasi.

Je,Kujamiana Huondoa Msongo wa Mawazo kwa Wanawake?

Je,Kujamiana Huondoa Msongo wa Mawazo kwa Wanawake?
Utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha State University cha Jijini New York nchini Marekani umesema ya kwamba manii ni nzuri kwa wanawake kwani huwaondolea msongo wa mawazo.Pia watafiti hao wamesema wanawake wanaofanya tendo la ndoa mara kwa mara bila kutumia kinga (mapenzi salama) wanakuwa na kiwango idogo cha msongo wa mawazo na hufanya vizuri katika vipimo vya akili.
Hali hii wamesema inatokana na manii kuwa na kemikali ambazo humfanya mtu kuwa vizuri kihisia, huongeza upendo/unyenyekevu, huchochea mtu kupata usingizi na huwa na angalau aina tatu za kemikali za kuondoa msongo wa mawazo (anti-depressants).
Utafiti huo uliofanywa kwa kuwahoji wanawake 293 kwa kufuatilia maisha yao ya kujamiana dhidhi ya afya za akili zao (mental health).Manii huwa na mchanganyiko wa kemikali aina ya cortisol ambayo huongeza upendo, kemikali aina ya esterone na oxytocin ambazo zote humfanya mtu kuwa vizuri  kihisia (elevates mood).
Pia huwa na homoni aina za thyrotropin releasing hormone ambayo huondoa msongo wa mawazo, melatonin ambayo huchochea usingizi na serotonin homoni inayoondoa msongo wa mawazo.
Kutokana kuwepo kwa mchanganyiko wa kemikali na homoni hizo kwenye manii, watafiti  Gallup na Burch pamoja na mtaalamu wa saikolojia  Steven Platek wamesema ya kwamba wanawake ambao hujamiana na wanaume bila kinga yoyote (mapenzi salama) wana asilimia ndogo ya msongo wa mawazo tofauti na wale wasiojamiana.
Matokeo muhimu ya utafiti huu ambao umechapishwa katika jarida la Archives of Sexual Behavior ni kwamba hata baada ya baadhi ya watafitiwa kuongeza kiwango chao cha kujamiana, wale ambao walikuwa hawatumii kinga yoyote walikuwa na kiwango kidogo cha msongo wa mawazo tofauti na wale ambao walikuwa wakitumia kinga kama kondomu wakati wa kujamiana.Pia wanawake hawa ambao hawakutumia kinga walikuwa na kiwango kidogo cha msongo wa mawazo tofauti na wale ambao hawakushiriki tendo la ndoa kabisa.
Hata wale wanawake ambao ni wasagaji na wana wapenzi wengi pia wameonekana kuwa na kiwango kikubwa cha msongo wa mawazo  kama wale wanawake ambao hawakushiriki tendo la ndoa kabisa.
Watafiti hao wamesema sio tu kujamiana huongeza furaha kwa mwanamke na hivyo kumuondolea msongo wa mawazo bali kiwango cha furaha pia huendana na wingi wa manii katika mili yao.
Utafiti huu usiwe chanzo cha watu kufanya mapenzi bila kinga bali uwe chanzo cha ufanya mapenzi salama na mwenza unayemuamini.Pia tunakemea na kupinga wale wote wanaofanya vitendo vya usagaji kwani ni hatari kwa afya zao kwani ni chanzo kimojawapo cha magonjwa ya akili.Tutakuletea makala ya uhusiano kati ya usagaji na ugonjwa wa akili.

Alhamisi, 19 Septemba 2019

KUCHAGUA JINSIA YA MTOTO

Je, unaweza kuchagua jinsia ya mtoto?

Kwa muda mrefu tukiwa tunazaa watoto, wanawake wamekuwa wakichangia mawazo jinsi ya kuongeza nafasi za kuzaa mtoto wa kike au kiume. Kwa bahati mbaya hakuna ushahidi wa matibabu kwamba yeyote kati hayo inaweza kufanya kazi!


Baada ya kusema hivyo, daima kutakuwa na mwanamama ambaye atakuambia hadithi za wazee ambayo alitumia. Kwa hiyo ikiwa unafikiria kujaribu kupata mtoto mwenye jinsia unayoitaka, kwa nini usijaribu baadhi ya mapendekezo hapa chini;
Uwezekano zaidi wa kumzaa mvulana kama:
  • Ukikutana kimwili na mwenza wako siku ya kupevuka kwa yai, kama inavofikirika manii kuogelea kwa kasi na kufikia yai kwanza.
  • Ukifika kileleni kabla ya mpenzi wako, hali hii inafungua kimiminika cha bezi kinachodhaniwa kua rafiki wa mbegu ya kiume zaidi kuliko asidi iliyopo kwenye uke.
  • Uume kupenya sana wakati wa tendo, kama vile kwa nyuma (doggy style).
  • Mpenzi wako ana idadi kubwa ya manii. Hii ni kwa sababu manii zinazo kubeba mbegu ya kiume hazina nguvu kama mbegu ya kike, na hivyo nafasi zaidi ya manii ya mbegu ya kiume kufikia yai kwanza inategemea wingi wa manii.
  • Epuka kujamiiana wiki moja kabla ya upevushwaji wa yai na kisha kufanya tendo mara moja kwenye siku ya upevushwaji, ili idadi ya manii iwe ya kutosha.
  • Mpenzi wako akipendekeza kufanya tendo la ndoa.
  • Kufanya tendo la ndoa wakati wa usiku.
  • Kujamiina siku isiyo ya kawaida ya mwezi.
  • Mpenzi wako ajiachie kwa kuweka sehemu zake za siri katika hali ya ubaridi kwa kuvaa boksa na suruali za kutosha kupitisha hewa.
  • Unakula vyakula vya chumvi, nyama nyingi, samaki, unga mweupe, pasta, matunda, mboga fulani, lakini kuepuka maziwa na bidhaa za maziwa, kama vile mtindi na jibini, karanga, chokoleti, samaki na mkate wote.
Uwezekano zaidi wa kumzaa msichana kama:
  • Kujamiiana mapema katika mzunguko wako, siku chache kabla ya siku yako ya kupevushwa yai. Hii ni kwa sababu manii ya kike yanadhaniwa kuwa imara na kwa hiyo hudumu zaidi kuliko mbegu ya kiume, ambaye itakufa kabla ya kufikia yai.
  • Mpenzi wako akifikia kileleni kabla yako.
  • Kujaamiana mara kwa mara ili kupunguza kiwango cha mbegu ya mpenzi wako, na hivyo kuongeza uwezekano wa mbegu ya kike kufikia yai kwanza.
  • Mwenza wako ahakikishe asipenye kwa kina sana [shallow penetration].
  • Kujaamiana pasipo kinga kwa siku nne hadi tano kabla ya upevushwaji wa yai, ili kupunguza nafasi ya manii ya kiume kufikia yai kwanza.
  • Mpenzi wako azidi kua na joto la kawaida katika sehemu zake za siri kwa kuvaa chupi na nguo nyepesi zinazomuachia mwili wake.
  • Pendekeza kufanya tendo la ndoa.
  • Pendekeza kufanya tendo la ndoa wakati wa mchana.
  • Pendekeza kujaamiana hata siku za kawaida za mwezi.
  • Kuna dhana ya kua unaweka kijiko cha mbao chini ya kitanda chako na uzi mwekundu chini ya mto wako.
Zingatia kunywa maziwa mengi na kula bidhaa za maziwa kama vile jibini na mtindi, vyakula visivyo na chumvi, mchele, pasta, baadhi ya mboga, maji ya madini, kiasi kidogo cha nyama na viazi, lakini epuka chumvi na vyakula vingine vya chumvi, divai na bia, matunda , mchicha, nyanya na uyoga, chokoleti, kahawa na chai.

MZUNGUKO WA HEDHI

JINSI YA KUHESABU MZUNGUKO WAKO WA HEDHI NA JINSI YA KUJUA SIKU YAKO YA HATARI YA KUPATA MIMBA
Leo kutana na Dr.Matimbwa katika kukuletea kwa mara nyingine tena maana nilishawahi toa darsa kama hili hapo mwanzo ila kutokana na unyeti wa suala hili basi nitalirudia kwa namna nyingine ili liweze kufahamika vizur.
Tuanze na somo letu.........
Siku za hatari za mwanamke ni zipi?
Hizi ni siku ambazo mwanamke akishiriki ngono bila kutumia kinga anapata ujauzito bila wasiwasi wowote labda kama ana matatizo yanayomfanya asibebe mimba au mwanaume wake ana matatizo.
Utazijuaje siku hizo?
Kwanza kabisa ili ujue siku zako za hatari lazima ujue idadi ya siku za mzunguko wako. Kuna aina tatu za mzunguko.. mzunguko mrefu ambao unachukua siku 35, mzunguko mfupi unaochukua siku 25 na ule wa kawaida unaochukua siku 28 na ndio mzunguko ambao watu wengi wanao.
Unajuaje mzunguko wako?
Hesabu siku tangu siku ile ya kwanza uliyoona siku zako za hedhi mpaka siku moja kabla ya kuona siku zako za hedhi zinazofuata. Unashauriwa uchukue miezi mitatu mpaka sita ukihesabu ili ue na uhakika kwamba mzunguko wa tarehe zako haubadiliki, kama umeshahesabu siku za nyuma kabla ya kusoma makala hii ni vizuri pia. Mfano umeanza kuona siku zako tarehe moja mwezi wa nne alafu ziko zako zingine ukaziona tarehe 29 mwezi wa nne, chukua 29 toa 1 utapata 28.. maana yake wewe unamzunguko wa siku 28.
SIKU YA UZAZI
#Kiundani Siku za uzazi ni siku ambazo kuna uwezekano mkubwa wa kupata mimba, ni siku 4 kabla ya siku ya yai kutoka/kupevuka.
Kawaida yai hupevuka siku 14 kabla ya ya siku ya bleed.
Hii ni siku muhimu sana kwa wana ndoa kuijua. Siku hii yai huwa linakuwa limeshakomaa na tayari limeshatoka katika nyumba yake ya mayai (ovaries) na kuelekea katika mirija ya uzazi (fallopian tube) tayari kukutana na mbegu ya kiume. Na kumbuka mbegu za kiume huishi muda wa masaa angalau 72 kwa hiyo muda wowote ndani ya masaa 72 kabla ya yai kutoka katika ovaries mtu na mke anaweza kudungwa mimba. Mfano kama yai linatoka tarehe 13, basi ukifanya tendo la ndoa siku ya tarehe 13,12,11,10 zote unaweza pata mimba - kwa hiyo hizi huitwa siku za mimba (fertile days), tofautisha na siku za hatari ambazo ni kuanzia siku yai limetoka na siku kadhaa baada ya yai kutoka.
KWA NINI BAADHI YA WANANDOA HUCHELEWA KUTUNGA MIMBA?
Kupata mtoto ni majaliwa ya mwenyezi Mungu lakini inaweza pia sababishwa na baadhi ya mambo kama vile yalivyoorodheshwa hapa chini. Hizi ni baadhi ya sababu, ili upate uhakika unatakiwa uende hospitalini na upime.
👉🏿1- MAISHA MAFUPI YA YAI LA KIKE.
Yai likitoka katika nyumba ya mayai na kuelekea mirija ya uzazi hadi kizazi linaweza ishi masaa kuanzia12 hadi 24+. Mfano yai limotoka saa1 asubuhi na wewe ukakutana na mwenza wako saa5 usiku. Ikiwa yai lako linauhai wa masaa12 hilo yai mbegu za kiume zitalikuta limesha pooza. Lakini kama lina uhai wa masaa 20 basi kuna uwezekano mkubwa wa kutunga mimba.
Nini cha kufanya kama unahangaika kupata mimba hakikisha unazitumia vizuri siku za uzazi, ikiwezekana fanya tendo la ndoa kila siku za hatari.
👉🏿2- MBEGU ZA KIUME HAFIFU/DHAIFU/CHACHE.
Mbegu zinaweza kuwa hazina mikia na hazina nguvu na haziwezi kuogelea hadi kuliwahi yai. Mshindo mmoja unaweza kutoa mbegu karibia au zaidi ya milioni40. Mbegu hizo hushindana ili kuliwahi yai, ni ile mbegu bora tu ndio itafika mapema.Kama mbegu ni chache (chini ya milioni 10 kwa mshindo mmoja) basi uwezekano wa kuwa na mbegu bora nyingi unakuwa mdogo.
👉🏿3- VIZUIZI KAMA UVIMBEE KWENYE MIRIJA YA UZAZI
Uvimbe unazuia yai na mbegu za kiume kukutana kirahisi. Uvimbe unaweza jitokeza kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na magonjwa na hali ya hewa au uvimbe tu usiojulikana kama endometriosis
👉🏿4- UCHACHU MKALI KWENYE UKE (ASIDI NYINGI)
uchachu mkubwa unaua mbegu nyingi za kiume, hivyo kupunguza idadi ya mbegu zenye uwezo wa kuliwahi yai.

👉🏿5- UCHAFU 
uchafu na ute mzito ndani ya kizazi huzifanya mbegu kushindwa kuogelea na kuwahi kurutubisha yai

👉🏿6- MALANGO WA UZAZI KUTOKUFUNGUKA (CERVIX)
 Mlango kati ya uke na mji wa mimba usipofunguka na kuruhusu mbegu kupita inachangia pia kuchelewa kupata ujauzito.
👉🏿7- MVURUGIKO WA HOMONI.
Baadhi ya homoni kutofanya kazi vizuri. Homoni ndio zinaamrisha mwili kufanya kazi zote za uzazi tangu kuamrisha yai litoke, lipasuke na pia lijishikize kwenye mji wa uzazi. Pia homoni ndio zinachochea viamshi vya tendo la ndoa. Kama homoni zimevurugwa basi mambo yako yatavurugika.
DALILI ZA SIKU ZA UZAZI
👆🏿1- UTE UTE UKENI - Ukikaribia siku zako za uzazi yaani yai ndio linajiandaa kutoka katika mji wa mayai basi kunakuwa na mabadiliko ya ute ukeni, siku za mwanzo kunakuwa na ute mzito, siku ya uzazi (yai limetoka) kunakuwa na ute unaonasa kama utauvuta unavutika na siku zinazofuata baada ya yai kutoka ute unakuwepo lakini unakuwa mgumu kama mtindi.
👆🏿2- JOTO KUONGEZEKA- Joto la mwili linaweza ongezeka kuanzia siku kabla yai halijatoka na linakuwa juu zaidi siku yai limetoka. Kama unapima joto pima asubuhi kabla hujaamka kitandani.
👆🏿3- MLANGO WA UZAZI KUWA LAINI – Mlango wa uzazi upo kati ya nyumba ya uzazi na uke. Mlango huu kawaida huwa mgumu kama pua, lakini siku yai likitoka unakuwa mlaini kama shavu au lips na pia hupanuka kidogo na kusogea zaidi kwenye uke. Wakati huu pia mlango huu huwa ni rahisi kufunguka.
👆🏿4- HAMU YA TENDO LA NDOA KUONGEZEKA – Wanawake wengi katika siku hizi huwa wachangamfu sana kwa tendo la ndoa. Mwanaume inatakiwa uwe mwelewa pindi mwenzio anapokusogelea uchangamke mana ukizubaa unapoteza ramani ya uzazi.
👆🏿5- MAZIWA KUWA LAINI.
👆🏿6- UWEZO WA KUNUSA VITU VINGI HUONGEZEKA – Wanawake wengi huwa na uwezo mkubwa wa kunusa na kuelewa harufu za vitu vingi sana wakati wakiwa period.
👆🏿7- MAUMIVU UPANDE MMOJA WA KIUNO – wengine pia hupata maumivu upande mmoja wa tumbo la uzazi. Kama dalili hii itaambatana na dalili zingine hapo juu na pia inaangukia siku ambayo umeikadiria ndiyo ya uzazi basi una uhakika hiyo ni ndio siku yenyewe.
👆🏿8- Kuna dalili nyingine nyingi lakini si za jumla kwa watu wengi zinakuwa kwa watu wachache wachache kama kuumwa kichwa na kujisikia vibaya
No photo description available.
JINSI YA KUHESABU SIKU ZA HATARI ZA KUSHIKA MIMBA
Naomba ieleweke kwamba wanawake wametofautiana kwa asilimia kubwa sana ktika mzunguko wao wa bleed hivyo kwa utangulizi tuu kuwa makini na jinsi unavyoanza bleed ili iweze kukusaidia katiaka kuhesabu kwako siku za hatari ..Na si kulinganisha siku ambayo labda ulianza sawa na rafiki yako....
1:16 days abnormal
2:18 days abnormal
3: 21 day cycle abnormal
4: 28 day cycle which is normal
5:30 days cycle which is normal
6: 32 days cycle which is normal
7: 33 , 35, 40 or more this is abnormal
Jinsi ya kuhesabu siku zako
mfano: umeanza kubleed leo tarehe 9 / 7/2017 kwa hiyo chukua daftari na andika na hesabu moja. hesabu kuanzia hapo mpaka utakapo fika 16 na ujua siku ya kumi na sita itaangukia tarehe ngapi? utakuja kuona siku ya 16 inaangukia tarehe 24/7/2017 hivyo hedhi nyingine itaanza 25/7/2017. hivyo hivyo utaanza kuhesabu kutoka tarehe 25/7/2017 mpaka kumi na sita na utakuja kungundua kuwa siku ya kumi na sita itakuwa ni tarehe 9/8/2017. hivyo inatakiwa uanze kubleed tarehe 10/8/2017. hivyo utakuwa unahesabu vivyo kila mwezi.
Hivyo basi wanawake wanaopata hedhi chini ya siku au siku 18 huwa wana matatizo hivyo wanatakiwa waende kumuona daktari kwani kitaalamu sio sahihi. hivyo ikitokea mke wako anableed kwa mzunguko wa siku 18 MPELEKE hospitali akapate ushari.
Angalizo: kuna wanawake wanaokuwa na mzunguko wa siku 24 au 26
[U]
WANAWAKE WANAOBLEED 28 DAYS HOW TO CALCULATE SAFE DATE AND SIKU ZA MIMBA KABLA YA SIKU YA HATARI
MFANO
UMEANZA KUPATA HEDHI TAHERE 9/7/2017 NA UNA MZUNGUKO WA SIKU 28
9, 10,11,12,13,14,15,16,17,18,19, 20,21,22,23,24,25,26,27,28,29, 30,31/JULY
1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 21 22 23
1, 2, 3, 4, 5/AUGUST
24 25 26 27 28
HIVYO HEDHI NYINGINE ITAKUWA TAREHE 6/AUGUST 2017
RED MEANS SIKU ZA HATARI
HIVYO BASI SIKU SALAMA NI BAADA YA DAMU KUKATA UNAWEZA KUANZA KUMTUMIA MAMA LAKINI IKIFIKA SIKU YA KUMI NA TATU YAI KUWA LIKO YATARI NA HUANZA KUSHUKA. KIPINDI HIKI MAMA HUTOKWA NA UTE MZITO WA KUNATA AMBAO HUWA NI DAWA KWA AJILI YA KULINDA NA KUTENGENEZA MJI WA MIMBA KUWA TAYARI KUPOKEA MBEGU ZA KIUME KWA AJIRI YA URUTUBISHO .HIVYO MBEGU ZA BABA HUWEZA HUSAFIRI KWA URAHISI ZAIDI KATIKA MAJI MAJI HAYA.
WANAWAKE WENYE SIKU 30
KWA MFANO, AMEANZA TAREHE 9/7/2017
9,10.11.12.13,14,15,16,17,18,1 9,20,21,22,23,24,25,26,27,28,2 9,30,31/JULY
1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 21 22 23
1, 2, 3, 4, 5, 6, 7 /AUGUST
24 25 26 27 28 29 30
HIVYO HEDHI NYINGINE ITAKUWA TAREHE 8/8/2017
ANGALIA TOFAUTI KATI YA MTU ANAYEBLEED KWA SIKU 28 NA 30. KIMSINGI, YAI HUCHUKUA SIKU KUMI NA NNE KUHARIBIKA BAADA YA KUKOSA KIRUTUBISHO. HIVYO HATA MWANAMKE AWE ANA MZUNGUKO WA 16,18,20,24,26,28.30.32.34 AU 40 AU ZAIDI. ITACHUKUA SIKU KUMI NA NNE ILI YAI LAKE LIWEKE KUHARIBIKA. NA SIKU YA KUMI NA TANO NDIO HUWA SIKU YA KWANZA KUANZA KUBLEED YAANI YAI LIMEKOSA KIRUTUBISHO.
VIVYO ANZA KUHESABU KUANZIA SIKU YA TAREHE 28 KURUDI NYUMA UTAKUTA KUWA SIKU YA KUMI NA NNE NI TAREHE 23. HIVYO SIKU YA HARATARI ITAKUWA TAREHE 22 LAKINI KWA KUWA YAI HUCHUKUA SAA 72 WAKATI LIKISUBIRI KIRUTUBISHO NDIO MAANA TUNAANZA NA SIKU YA 13 , 14, 15 TOKEA PALE ULIPOBLEED.
NA KWA MWANAMAMA ANAYECHUKUA SIKU 30 UKIHESABU KUANZIA 30 KURUDI NYUMA UTAGUNDUA KUWA SIKU YA 14 NI TAREHE 25/7
HIVYO SIKU YA HATARI NI TAREHE 24/7 NA KWA SABAU YAI HUKAA SIKU TATU HIVYO TAREHE 23,24, NA 25/7 /2017 AMBAZO NI SAWA NA SIKU YA 16, 17, NA 17 KATIKA KUHESABU CYCLE
YULE WA SIKU THELATHINI NA MBILI ITAKIWA SIKU YA HATARI NI YA 18 NA SIKU ZAKE TATU ZA HATARI NI 17, 18 NA 19 AMBAZO TAREHE 25,26,27/JULY KAMA SIKU ZAKE ZA HATARI......
TANBIHI:
Ninaposema:-
#Abnomal namaanisha si hali ya kawaida/Chini ya
#Normal namaanisha katika hali yake ya kawaida.
#More than Abnomal namaanisha ni zaidi ya hali yake ya kawaida.
#Bleed namaanisha ile siku ambayo damu za hedhi zinatoka.