SHINGO YA KIZAZI NI NINI?
♦ Shingo ya kizazi ‘cervix’ ni sehemu ya kizazi kati ya uke na mji wa mimba.
Sehemu hii ina kazi nyingi ikiwemo;
Sehemu hii ina kazi nyingi ikiwemo;
- Kupitisha mbegu za kiume kuelekea katika mji wa uzazi na hatimaye mirija ya uzazi ili kupevusha yai,
- Kupitisha damu ya hedhi
- Mlango anaopitia mtoto wakati wa kuzaliwa.
SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI
♦ Hii ni aina ya saratani inayoshambulia seli/chembechembe zilizoko ndani ya ngozi laini inayozunguka shingo ya kizazi.
NINI CHANZO CHAKE
♦ Husababishwa na aina ya virusi kinachoitwa ‘Human Papilloma Virus’ (HPV), kirusi hiki huambukizwa kwa njia ya kujamiiana na mtu mwenye maambukizi.
♦ Kuna tabia au hali hatarishi ambazo zinachangia mtu kupata saratani ya shingo ya kizazi, tabia/vitu hivyo ni pamoj ana;
- Kuanza ngono katika umri mdogo (chini ya miaka 18).
- Uvutaji wa sigara.
- Kuwa na wapenzi wengi au kujamiiana na mtu mwenye wapenzi wengi.
- Matumizi ya mafuta mengi kwenye chakula au kula vyakula vyenye mafuta kwa wingi.
- Kutokula mboga za majani na matunda.
- Upungufu wa kinga mwilini.
DALILI ZA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI
♦ Saratani ya shingo ya kizazi huanza na kuendelea kwa muda mrefu bila kuonesha dalili zozote.
Dalili ambazo zinaweza kujitokeza wakati ugonjwa upo katika hatua za mwisho ni pamoja na;
1. Kutokwa na damu isiyo ya hedhi ukeni.
- Kutokwa na damu ukeni baada ya kujamiiana.
- Kutokwa na damu ukeni kwa wanawake waliokwisha kukoma hedhi.
- Damu iliyochanganyikana na majimaji ya uke.
- Matone ya damu au damu kutoka kipindi kisicho cha hedhi.
3.Maumivu wakati wa kujamiiana
4.Maumivu chini ya tumbo, nyonga na kiunoni.
5.Kukojoa mkojo wenye damu,
6.Kupitisha mkojo na haja kubwa kwenye uke na
7.Upungufu wa damu.
NAMNA YA KUGUNDUA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI
♦ Saratani ya shingo ya uzazi huchukua muda mrefu mpaka kuonesha dalili.
♦ Vipimo vya uchunguzi vinavyofanyika ni pamoja na;
- Pap Smear - Kipimo hiki ni rahisi na hakina madhara yoyote. Inashauriwa kufanya kipimo hiki mara moja kwa mwaka.
- Colposcopy - Hiki ni kipimo kinachotumia darubini kuangalia chembechembe/ seli zilizondani ya ngozi inayozunguka shingo ya uzazi.
♦ Matibabu ya saratani hutolewa kulingana na hatua ya ugonjwa.
♦ Ugonjwa ukiwa hatua za mwanzo huweza kutibika kabisa (ingawa kuna uwezekano wa kujirudia).
♦ Hatua za mwisho za ugonjwa huu huwa haziwezi kupona kabisa. kinachofanyika mara nyingi ni kutoa matibabu yatayotuliza dalili na maumivu na kumuwezesha mgonjwa kuishi vizuri.
♦ Huduma za matibabu hutolewa kwa njia zifuatazo:
- Upasuaji katika hatua za mwanzo za ugonjwa.
- Mionzi.
- Dawa za Saratani.
- Mionzi pamoja na dawa za saratani.
♦ Kupata chanjo ya ‘Human Papilloma Virus’.
♦ Kuepuka ngono katika umri mdogo.
♦ Kuwa na mwenzi mmoja mwaminifu.
♦ Kutumia kondomu kila mara unapojamiiana.
♦ Epuka kuvuta sigara.
♦ Kufanyiwa uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi angalau mara moja kwa mwaka.
♦ Tibu kikamilifu magonjwa ya ngono (STI).
♦ Punguza matumizi ya mafuta mengi kwenye chakula
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni