Ijumaa, 7 Februari 2020

UMUHIMU WA WATOTO KULALA MCHANA


Wazazi wengi huwalazimisha watoto kulala mchana bila kujua umuhim wa kufanya ivo, wengine hawajui na wala hawafanyi jitihada za kuwalaza watoto mchana. Wengine hufanya ivo kupunguza vurugu na mikimiki ya watoto, Wengine wanafanya kwa sababu ya mazoea, kuiga kwa majirani na sababu nyingi zingine. Tambua umuhim wa mtoto kulala mchana;
  • Husaidia ukuaji wa mtoto hasa wa ubongo na viungo vya mwili
  • Inaongeza ubunifu na ufanisi katika shule na maeneo mengine
  • Inaongeza uwezo wa kujifunza na kumbukumbu
  • Inapunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo
Kwa sababu izo ni muhimu sana wazazi kuhimiza watoto kulala mchana kwaajili ya afya bora na ukuaji bora. Tunaweza kutoona faida yake mara moja lakini baadae tukaona matokeo  makubwa hasa kwenye ukuaji wao na uwezo wa akili zao darasani, fikra zao na mambo yanayoendana na kuepuka magonjwa kama vile ya moyo. Mhimize mtoto alale mchana kwaajili ya afya bora.

Jumatano, 5 Februari 2020

NJIA ZA KUZUIA KUTAPIKA WAKATI WA UJAUZITO



Kutapika kwa mama mjamzito inaleta kero na mama huyo kukosa raha mara nyingi. Miezi ya awali ya ujauzito hua na changamoto hii sana lakini ikiendelea inaleta karaha kabisa, unaweza kuzuia hali hii kwa njia zifuatazo.
  • Kula matunda au mkate wa kukaushwa asubui
  • kunywa vinywaji nusu saa kabla ya kula au baada ya kula. Usile na kunywa kwa wakati mmoja.
  • Kunywa maji mengi sana kuzuia upungufu wa maji mwilini (dehydration). Jitaidi kunywa lita 2.5 kila siku na pamoja na juisi ya matunda.
  • Epuka kulala baada ya chakula
  • Pata muda wa kupumzika wa kutosha na pata kusinzia mchana
  • Fanya mazoezi
  • Ndimu na tangawizi husaidia kupunguza na kuondoa kichefuchefu. Unaweza kunywa juisi ya ndimu au tikiti maji.
  • Epuka kupita sehemu yenye harufu ya chakula
  • Epuka kula vyakula vyenye pilipili au viungo vingi
  • Pata hewa (Oxygen) ya kutosha na fungua madirisha ili hewa iweze kuingia
  • Usiache kula au kuruka milo.
Hizo ni kati ya njia chache za asili kati ya nyingi. Tatizo likizidi muone daktari kwa matibabu zaidi na vipimo zaidi

Muda unaofaa kubeba mimba baada ya mimba uliyobeba kuharibika?

Ni vizuri kwanza kujua vitu vinavyoweza kusababisha mimba kuharibika.
Mimba nyingi huharibika kutokana na makosa ya ukuaji wa mtoto. Sehemu kubwa ya makosa haya huwa ni kwenye vinasaba vyake. Yanaweza kuwa ya kurithi au yasiyo ya kurithi yaliyotokea kwa bahati mbaya kwa mtoto.
Zipo pia sababu nyingine kama vile maumbile ya viuongo vya uzazi, magonjwa ya mama kama vile kisukari, magonjwa ya damu, magonjwa ya vijidudu (infection).
Pamoja na sababu za mimba kuharibika kuwa nyingi, mara nyingi linapotokea tatizo hili huwa sababu iliyosababisha haifahamiki. Hali hii husababisha akinamama wengi na wenza wao kubaki na maswali mengi kwanini imewatokea hivyo na hujiuliza kama inaweza kutokea tena kwenye ujauzito mwingine.
Mara nyingi hali hii hutokea mara moja na haijirudii. Hii ni kwa sababu makosa ya ukuaji yanayotokea bahati mbaya huwa ni jambo lenye uwezekano mdogo sana kujirudia. Hata hivyo iwapo ujauzito umeharibika kwa sababu nyingine kama vile za kimaumbile au magonjwa ya damu, uwezekano wa kujirudia huwa mkubwa iwapo hali hiyo haijagundulika na hatua stahiki kuchukuliwa.
Kujibu swali la msingi ni baada ya muda gani inafaa kubeba mimba nyingine, inategemea kama ni mara ya kwanza ujauzito kubadilika au ni hali iliyojorudia. Kama ni mara ya kwanza, unaweza kubeba ujauzito mwingine mara tuu unapopata siku zako (vizuri zaidi angalau baada ya wiki 6 baada ya ujauzito kuharibika). Kwa kipindi hiki mwili unakuwa tayari kupokea ujauzito mwingine.
Hata hivyo kwa vile swala la ujauzito kuharibika linapokelewa kwa hisia tofauti na linaowakuta, ni vizuri ukabeba ujauzito baada ya kuwa umeshakuwa katika hali ya kawaida kihisia.


Iwapo ujauzito kuharibika sio mara ya kwanza, kuna umuhimu wa kufanyiwa vipimo na daktari ili upewe ushauri juu ya kujiandaa na ujauzito mwingine. Aina ya ushauri inategemea na matokeo ya vipimo atakavyoshauri daktari. Vilevile inategemea kama ujauzito (mtoto) ulioharibika ulikutwa na tatizo lolote linalohitaji muda kulichunguza. Vipimo hivi vinaweza kuwa pamoja na vipimo vya damu, kipimo cha ultrasound na vingine.
Daktari anaweza kushauri utumie dawa za folic acid au vitamin wakati ukijiandaa na ujauzi mwingine.
Wanawake wengi (asilimia 70) waliopata tatizo la ujauzito kuharibika walifanikiwa kupata ujauzito tena na kujifungua watoto wenye afya njema. Kwahiyo usikate tamaa iwapo umekutwa na hali hii.

Njia thabiti ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU)

VVU/Ukimwi umeendelea kuwa ni moja kati ya changamoto kubwa katika sekta ya Afya duniani haswa kwa nchi zinazoendelea. Kutokana na Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), inakadiriwa kuwa, kuna watu milioni 36.9 wanaishi na virusi vya ukimwi duniani kote.
Kwa siku za karibuni, kumekuwa na matokeo chanya kwenye mapambano na ugonjwa wa ukimwi, sasa hivi watu wenye virusi vya ukimwi (VVU) wanaishi maisha yenye afya njema na kwa muda mrefu kwa msaada wa dawa za kufubaza makali ya virusi vya ukimwi (antiretroviral therapy (ART)), pia matumizi sahihi ya dawa hizi husaidia kupunguza muendeleo wa uabukizaji kwa wengine.



Kazi kubwa pia imefanyika ili kuzuia na hata kumaliza kabisa maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa kujifungua.
Ingawa kuna matokeo yote hayo chanya, lakini bado kuna sehemu kubwa ya jamii bao haina uelewa juu ya ugonjwa huu, hivyo TanzMED itakuwa inakuletea dondoo chache juu ya ugonjwa huu;
1. VVU vinaweza kuambukizwa kwa njia mbalimbali kama;
  • Kuambukizwa kwa mtoto mchanga wakati akiwa tumboni, wakati wa kuzaliwa au kwa kunyonyeshwa na mama anayeishi na virusi vya ukimwi. Hivyo, kabla na baada ya kuanza kubeba ujauzito, inashauriwa kupima Afya na kuhudhuria vyema kliniki kwa ajili ya vipimo na ushauri juu na njia za kuondoa maambukizi haya.
  • Kujamiiana bila ya kinga na mtu mwenye virusi vya ukimwi
  • Kuwekewa damu yenye virusi vya ukimwi
  • Kushare vitu vyenye incha kali (sindano, viwembe, masjine za kuchorea tattoo, mikasi nk) vilivyo na virusi vya ukimwi. Watumiaji wa madawa ya kulevya wapo kwenye hatari ya kuambukizana kwakuwa wengi hutumia sindano kwa pamoja
  • Matumizi ya vifaa vya upasuaji ambavyo havijafanyiwa usafi wa kuua virusi
2. Jinsi ya kujikinga au kuzuia maambukizi ya virusi vya ukiwmi (VVU) kwa wengine
  • Hakikisha unatumia zana pindi unapofanya ngono
  • Nenda kapime na upate tiba ya magonjwa mengine ya zinaa kwani kuwa na magonjwa ya zinaa kuna uwezekano mkubwa wa kuambukizwa virusi vya ukimwi, pia kupima na kujijua mapema, kunasaiia kulinda afya yako na kuzuia kuwaambukiza wengine
  • Hakikisha damuunayowekewa imepimwa na haina virusi vya ukimwi
  • Kutahiriwa kwa wanamume kunasaidia kupunguza maambukizi 
  • Matumizi ya mapema na yaliyobora ya dawa za kufubama makali ya virusi vya ukimwi (ARV) husaidia kukufanya uishi na afya bora pia kupunguza maambukizi kwa wengine
  • Kuishi maisha yanayompendeza mungu kwa kuacha kuzini kabla na nje ya ndoa

Jumatatu, 3 Februari 2020

Msongo wa Mawazo (Sonona)

Msongo wa mawazo ni mfadhaiko wa akili anaoupata mtu kutokana na shida, taabu, dhiki, matatizo au changamoto zinazomkabili katika maisha ya kila siku. Mtu hupata msongo wa mawazo pale anaposhindwa au kukosa namna ya kukabiliana na jambo linalomsumbua.



Vitu Vinavyosababisha Mtu Kupata Msongo wa Mawazo 
Kuna sababu nyingi zinazosababisha mtu kupata msongo wa mawazo, baadhi ya sababu hizo ambazo zimegawanyika katika makundi mawili ambayo ni kibiologia na kisaikolojia.

Sababu za kibiologia 
o Mtu kurithi vinasaba kutoka kwa mzazi/ wazazi 
o Magonjwa ya muda mrefu kama UKIMWI, figo, ini, moyo nk. 

Sababu za kisaikolojia 

  • Matukio yasiyofurahisha kama Ubakaji,Uvamizi, Ajali au Kufiwa, au kutekwa nyara  
  • Majanga kama Kimbunga, Mafuriko, Tetemeko la ardhi n.k 
  • Changamoto za kila siku za maisha Ugoni, Talaka, Mimba kuharibika, Kutoa mimba, Kutengana,       Kufungwa, Kuuguza au Kukosa kazi. 
  • Matatizo sehemu za kazi Kufukuzwa kazi / Chuo, Migogoro kazini au Kustaafu kazi. 
  • Mambo ambayo yanategemewa mtu kufurahi yanaweza kumsababishia msongo wa mawazo kama     Kuoa au Kuolewa, Kuzaliwa mtoto, Kufaulu mtihani, Ajira mpya, kuhamia nyumba mpya, Kupata ujauzito nk
Dalili za Msongo wa Mawazo 
  • Maumivu ya sehemu mbalimbali za mwili hasa kichwa na kifua
  • Kuwa na huzuni na kujisikia mnyonge
  • Kusahau na kukosa uwezo wa kufikiri vyema
  • Kujihisi kuchoka na kukosa ari nya kufanya kazi, 
  • Kuwa na hofu na kutokujiamini 
  • Kushindwa kufanya maamuzi sahihi,
  • Kushindwa kula au kula sana,
  • Kukosa hamu ya tendo la ndoa
  • Kupungua uzito au kuongezeka uzito 
  • Kubadilika kwa siku za hedhi au kutokuona kabisa 
  • Kulala muda mfupi na muda mwingi kuwa macho usiku 
  • Kukosa choo kwa muda mrefu 
  • Kutaka kujiua au kuwa na mawazo ya kujiua
Athari za Msongo wa Mawazo 
Athari za Msongo wa Mawazo zinaweza kuwa za kihisia au kitabia 

Athari za Kihisia 
  • Kuwa na hofu kupita kiasi 
  • Kuwa na mfadhaiko na 
  • Kuwa na hisia za kukosa ulinzi 
  • Kusahau na kushindwa kufikiria ipasavyo 
  • Kukosa utulivu na kuwa na huzuni.
Athari Kitabia 
  • Kula sana/-kushindwa kula 
  • Kubagua aina za vyakula. 
  • Kuwa na hasira 
  • Kunywa pombe kupita kiasi au Kutumia madawa ya kulevya, 
  • Kupenda kuwa mwenyewe na kujitenga na jamii 
  • Kuwa na huzuni na kulia 
  • Kutoelewana na jamii
Namna ya kupunguza Msongo wa Mawazo 
  • Tafuta chanzo cha msongo na epuka nalo au kubaliana nalo. 
  • Kuwa na mtizamo chanya kwamba hiyo changamoto inayokukabili kwani huo sio mwisho wa maisha.
  • Fanya mazoezi ili kupunguza mzigo wa hisia unaokuelemea na huondoa msongo wa mawazo. 
  • Epuka kuwa peke yako, washirikishe watu wa karibu matatizo yako kwa kuomba ushauri 
  • Pata muda wa kutosha wa kupumzika ikiwa ni pamoja na kulala 
  • Epuka mazoea mabaya kama kunywa pombe au kutumia dawa kwa imani kwamba zitakupunguzia msongo wa mawazo 
  • Jitahidi Kula vizuri kwani mwili unategemea chakula ili uweze kufanya kazi vizuri 
  • Fanya vitu ambavyo vitakupa starehe kama kusoma vitabu, kusikiliza mziki, kwenda sehemu za burudani, na kuwa na mtu wa kukufariji.
  • Badilisha mazingira kwa kutembelea sehemu mbalimbali kama vile fukwe za bahari, mbuga za wanyama, bustani nk
  • Pata ushauri wa wataalam (daktari, mwanasaikolojia nk) 
  • Kutumia dawa kwa usahihi kila wakati na 
  • Kuhudhuria kiliniki kila wakati kama ulivyopangiwa na wataalam wa afya.

IJUE SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI


SHINGO YA KIZAZI NI NINI?

 ♦ Shingo ya kizazi ‘cervix’ ni sehemu ya kizazi kati ya uke na mji wa mimba. 

Sehemu hii ina kazi nyingi ikiwemo;   

  • Kupitisha mbegu za kiume kuelekea katika mji wa uzazi na hatimaye mirija ya uzazi ili kupevusha yai,
  • Kupitisha damu ya hedhi 
  • Mlango anaopitia mtoto wakati wa kuzaliwa.





 SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI 
♦ Hii ni aina ya saratani inayoshambulia seli/chembechembe zilizoko ndani ya ngozi laini inayozunguka shingo ya kizazi. 

 NINI CHANZO CHAKE 
♦ Husababishwa na aina ya virusi kinachoitwa ‘Human Papilloma Virus’ (HPV), kirusi hiki huambukizwa kwa njia ya kujamiiana na mtu mwenye maambukizi. 

♦ Kuna tabia au hali hatarishi ambazo zinachangia mtu kupata saratani ya shingo ya kizazi, tabia/vitu hivyo ni pamoj ana; 

  • Kuanza ngono katika umri mdogo (chini ya miaka 18). 
  • Uvutaji wa sigara. 
  • Kuwa na wapenzi wengi au kujamiiana na mtu mwenye wapenzi wengi. 
  • Matumizi ya mafuta mengi kwenye chakula au kula vyakula vyenye mafuta kwa wingi. 
  • Kutokula mboga za majani na matunda. 
  • Upungufu wa kinga mwilini.



DALILI ZA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI 
♦ Saratani ya shingo ya kizazi huanza na kuendelea kwa muda mrefu bila kuonesha dalili zozote. 

Dalili ambazo zinaweza kujitokeza wakati ugonjwa upo katika hatua za mwisho ni pamoja na;
 1. Kutokwa na damu isiyo ya hedhi ukeni. 

  • Kutokwa na damu ukeni baada ya kujamiiana. 
  • Kutokwa na damu ukeni kwa wanawake waliokwisha kukoma hedhi. 
  • Damu iliyochanganyikana na majimaji ya uke. 
  • Matone ya damu au damu kutoka kipindi kisicho cha hedhi.
 2. Kutokwa na majimaji au uchafu ukeni wenye harufu mbaya wakati mwingine ukiwa umechanganyika na damu. 
3.Maumivu wakati wa kujamiiana 
4.Maumivu chini ya tumbo, nyonga na kiunoni. 
5.Kukojoa mkojo wenye damu, 
6.Kupitisha mkojo na haja kubwa kwenye uke na 
7.Upungufu wa damu.


 NAMNA YA KUGUNDUA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI 
♦ Saratani ya shingo ya uzazi huchukua muda mrefu mpaka kuonesha dalili. 

♦ Vipimo vya uchunguzi vinavyofanyika ni pamoja na; 

  • Pap Smear - Kipimo hiki ni rahisi na hakina madhara yoyote. Inashauriwa kufanya kipimo hiki mara moja kwa mwaka. 
  • Colposcopy - Hiki ni kipimo kinachotumia darubini kuangalia chembechembe/ seli zilizondani ya ngozi inayozunguka shingo ya uzazi. 
 MATIBABU 
♦ Matibabu ya saratani hutolewa kulingana na hatua ya ugonjwa. 
♦ Ugonjwa ukiwa hatua za mwanzo huweza kutibika kabisa (ingawa kuna uwezekano wa kujirudia). 
♦ Hatua za mwisho za ugonjwa huu huwa haziwezi kupona kabisa. kinachofanyika mara nyingi ni kutoa matibabu yatayotuliza dalili na maumivu na kumuwezesha mgonjwa kuishi vizuri. 

Huduma za matibabu hutolewa kwa njia zifuatazo: 

  • Upasuaji katika hatua za mwanzo za ugonjwa.
  •  Mionzi.
  •  Dawa za Saratani.
  •  Mionzi pamoja na dawa za saratani.
NAMNA YA KUJIKINGA NA SARATANI YA SHINGO YA UZAZI 
♦ Kupata chanjo ya ‘Human Papilloma Virus’. 
♦ Kuepuka ngono katika umri mdogo. 
♦ Kuwa na mwenzi mmoja mwaminifu. 
♦ Kutumia kondomu kila mara unapojamiiana. 
♦ Epuka kuvuta sigara. 
♦ Kufanyiwa uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi angalau mara moja kwa mwaka. 
♦ Tibu kikamilifu magonjwa ya ngono (STI). 
♦ Punguza matumizi ya mafuta mengi kwenye chakula

Alhamisi, 9 Januari 2020

FAHAMU KUHUSU BAWASIRI /HAEMORRHOIDS





Bawasiri (Haemorrhoids) ni uvimbe ambao unaweza kutokea katika njia ya haja kubwa  (anus) na  sehemu ya mwisho ya  puru(rectum). Tatizo hili huwakumba wengi na wengi wao hua na aibu katika kulielezea au kwenda katika vituo vya afya kwa matibabu zaidi.
Kuna mishipa ya damu inayopita ndani  ya njia ya haja kubwa (anus) na sehemu ya chini ya puru (rectum) ijulikanayo kama vena.
Hii mishipa  mara nyingine huwa mipana na kujaa  damu zaidi kuliko kawaida hali ambayo huweza kupelekea uvimbe uitwao bawasiri.
Bawasiri husababishwa na vitu vifuatavyo:-

  1. Kupata haja/kinyesi kigumu
  1. Ujauzito
  1. Uzito kupita kiasi
  1. Kufanya ngono kwa njia ya haja kubwa
  1. maumivu/usumbufu
  1. kupata uvimbe katika eneo la haja kubwa
  1. kujitokeza kwa vinyama wakati wa haja kubwa
  1. kuwashwa katika eneo la haja kubwa
  1. kuwa na hisia za haja kubwa hata baada ya kujisaidia
Hakikisha unapata choo la laini wakati wote, Hivyo unaweza kufanya yafuatayo.
  • Kula mboga za majani, matunda na nafaka kwa wingi
  • Kunywa maji ya kutosha kila siku glasi 4-8 kwa siku
  • Kujisaidia kwa wakati pindi unapohisi haja
  • Punguza kukaa muda mrefu chooni

Dalili
Dalili zinaweza kutofautiana. Haemorrhoids ndogo kwa kawaida haina maumivu.
Matibabu
Lakini pia kuna dawa ambazo unaweza kupaka au kuingiza kwenye njia ya haja kubwa kwa ajili ya kupunguza maumivu au dalili unazozisikia.

Matibabu mengine ni upasuaji (hermorrhoidectomy na stapled hermorrhoidopexy)




Jumatatu, 6 Januari 2020

FAHAMU KUHUSU FISTULA/NASURI KWA WANAWAKE


kitaalamu ni tundu ambalo silo la kawaida linaloonganisha viungo viwili vya binadamu, kwa kawaida viungo vya binadamu havina matundu lakini matundu haya yanapotokea huitwa fistula, mfano tundu kati ya koo la hewa na chakula, tundu kati ya uke na njia ya choo, tundu kati ya njia ya uke na mkojo.
fistula ya uzazi hutokea pale panapokua na tundu kati ya njia ya choo kubwa, choo ndogo na uke au njia ya uzazi...hali hii husababisha kinyesi na mkojo kupita sehemu za siri.


fistula husababishwa na nini?
kwa nchi ambazo hazijaendelea kama tanzania fistula husababishwa na 
1. Uchungu wa muda mrefu ambapo mtoto anakandamiza kibofu cha mama au utumbo mkubwa na kusababisha damu kushindwa kufika eneo hilo na kuoza au kuchanika, hali hii ndio huleta tundu hilo la fistula.

sababu zingine ni kuvunjika kwa mifupa ya mapaja, saratani mbalimbali za uzazi,kubakwa,kutoa mimba au makosa wakati wa upasuaji wa kizazi, mionzi ya matibabu ya kansa, magonjwa ya zinaa kama kaswende, ugonjwa wa kichocho


dalili za fistula ni zipi?

  • Kutokwa na mkojo au choo kubwa sehemu za siri hasa wakati wa usiku bila Kujitambua au kushindwa kuzuia.
  • Harufu kali sehemu za siri
  • Kuugua ugonjwa wa njia ya mkojo mara kwa mara maarufu kama uti
  • Maumivu makali ya uke na sehemu zinazozunguka
  • Maumivu makali wakati wa tendo la ndoa
  • Msongo wa mawazo
  • Kukosa siku za mwezi
  • Kuharibika kwa mimba zijazo
  • Ugonjwa wa ngozi sababu ya mkojo kumwagikia ngozi


Vipimo gani hufanyika kugundua fistula?
kipimo cha picha ya utrasound hutumika sana kuangalia kama kuna tundu ambalo sio la kawaida limetokea kwenye sehemu hizo za siri.

Matibabu ya fistula.
fistula ikigundulika mapema huweza kutibiwa kwa kuingiza mpira wa mkojo kitaalamu kama catheter na kuuacha hapo mpka tundu lile litakapoziba, mpira huweza kubadilishwa kulingana na na muda mgonjwa atakaotibiwa, dawa za kuua bacteria hutolewa na mgonjwa huwekewa drip za maji mengi ili kuongeza damu katika eneo husika kitu ambacho husaidia kupona haraka.
matibabu yakichelewa mgonjwa hutakiwa kufanyiwa opasuaji na daktari bingwa ili kushona tundu hilo, kwa hapa tanzania upasuaji huo ni bure kabisa katika hospitali ya CCBRT dar es laam.

Madhara ya fistula ni yapi?

  • kibovu cha mkojo kuondoka sehemu yake
  • kupata ugonjwa wa njia ya mkojo mara kwa mara
  • ugumba
  • kuishiwa damu
  • sehemu za uke wa mwanamke kuharibika
  • kuvunjika kwa ndoa
  • kutengwa na jamii
  • kujiua kwa wahanga wa tatizo hili.

jinsi gani tunaweza kuzui fistula kwenye jamii zetu?
  • kuzuia wasichana wadogo kuza
  • Ahakikisha mama hakai na uchungu zaidi ya masaa 12 baada ya uchungu kuanza
  • hakikisha mama anazalia hospitali ili asaidiwe vizuri
  • kuweka miondominu mizuri kwa ajili ya kusafirisha wagonjwa.

Alhamisi, 2 Januari 2020

Madhara ya kunyonya UUME/UKE





Kumekua na ongezeko la kitendo hiki kwa vijana na imekua kama ni sehemu ya mahaba kwa wapenzi hata inafikia hatua mwanaume ANAONA MKE/MPENZI WAKE HAJUI MAHABA KAMA HAJAMNYONYA UUME AU MWANAMKE KUONA HIVO ASIPONYONYWA YEYE.VILIVILE KUNA WANAWAKE WANAONA KUFANYA MAPENZI BILA KUNYONYA NI USHAMBAKitendo hiki ni pale mwanamke anapoweka uume wa mwenza wake mdomoni mwake na kuanza kunyonya kama pipi au mwanaume kuingiza ulimi ukeni pamoja na kunyonya via vya mwanamke pindi wapenzi hawa wawapo faragha.
kwa ufupi madhara hayo ni
1. KISONONO CHA KOO
2. KUBADILISHANA BACTERIA
3. FANGASI YA MDOMONI/KOO
4. VIDONDA MDOMONI
5. KUWEKA UWEZEKANO WA KUPATA KANSA YA KOO/ULIMI/MDOMO