Bawasiri (Haemorrhoids) ni uvimbe ambao unaweza kutokea katika njia ya haja kubwa (anus) na sehemu ya mwisho ya puru(rectum). Tatizo hili huwakumba wengi na wengi wao hua na aibu katika kulielezea au kwenda katika vituo vya afya kwa matibabu zaidi.
Kuna mishipa ya damu inayopita ndani ya njia ya haja kubwa (anus) na sehemu ya chini ya puru (rectum) ijulikanayo kama vena.
Hii mishipa mara nyingine huwa mipana na kujaa damu zaidi kuliko kawaida hali ambayo huweza kupelekea uvimbe uitwao bawasiri.
Bawasiri husababishwa na vitu vifuatavyo:-
- Kupata haja/kinyesi kigumu
- Ujauzito
- Uzito kupita kiasi
- Kufanya ngono kwa njia ya haja kubwa
- maumivu/usumbufu
- kupata uvimbe katika eneo la haja kubwa
- kujitokeza kwa vinyama wakati wa haja kubwa
- kuwashwa katika eneo la haja kubwa
- kuwa na hisia za haja kubwa hata baada ya kujisaidia
- Kula mboga za majani, matunda na nafaka kwa wingi
- Kunywa maji ya kutosha kila siku glasi 4-8 kwa siku
- Kujisaidia kwa wakati pindi unapohisi haja
- Punguza kukaa muda mrefu chooni
Dalili
Dalili zinaweza kutofautiana. Haemorrhoids ndogo kwa kawaida haina maumivu.
Matibabu
Lakini pia kuna dawa ambazo unaweza kupaka au kuingiza kwenye njia ya haja kubwa kwa ajili ya kupunguza maumivu au dalili unazozisikia.
Matibabu mengine ni upasuaji (hermorrhoidectomy na stapled hermorrhoidopexy)